HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 29 May 2017

HOSPITALI YA MKURANGA YAKABILIWA NA CHANGAMOTO-DK.KIGWANGALA

Na Chalila Kibuda ,Globu ya  Jamii
Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga inakabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana kuanzishwa kwake kulianzia katika zahanati.
Hayo ameyasema na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala wakati alipofanya ziara katika Hospitali ya Wilaya ya  Mkuranga,  amesema Hospitali ya Mkuranga kuanzia majengo kuwa mbalimbali tofauti na inavyotakiwa.
Amesema katika ziara hiyo amesema hata mfumo wa kuhifadhi taka katika hospitali hiyo hauko sawa pamoja  na hali ya usafi katika wodi ya wazazi.
Dk.Kigwangala amesema kutokana na mazingira yaliyopo katika hospitali itachukua hatua katika kuiweka hospitali hiyo kwenye .ubora mzuri.
Aidha amesema Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amekuwa bega kwa bega na hospitali ya  Mkuranga  ikiwa ni pamoja na kutafuta wadau katika kusaidia hospitali katika maeneo mbalimbali.
Dk. Kigwangala amesema kuwa Mganga Mkuu wa Hospitali  kujitoa katika kufanya masuala mengine bila kusubiri serikali kuu ikiwa ni pamoja na kutenga siku ya kufanaya  usafi katika hospitali hiyo.
Nae Mbunge wa  Mkuranga , Abdallah Ulega amesema ziara ya Naibu Waziri huyo itazaa matunda kwa hospitali ya Mkuranga kuwa na sifa ya hospitali ya Wilaya.
Amesema  watakuwa na utaratibu wa kufanya usafi kwa mara moja kwa wiki hali ambayo inaweza kuleta mabadiliko katika hospitali hiyo.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangalla akizungumza na watendaji wa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga na Halmashauri wakati ziara yake katika Hospitali hiyo. .(picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii).
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga akizungumza na watendaji wa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga na Halmashauri katika ziara ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala.
 Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akitoa neno la shukurani kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala kufanya ziara katika hospitali hiyo.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala akikabidhi gari la wagonjwa na vifaa kwa  Uongozi wa Wilaya ya Mkuranga
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala akitembelea na kukagua wodi mbalimbali katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga katika ziara yake aliyofanya katika Hospitali hiyo. (Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii).
 Sehemu ya vifaa vilivyokabidhiwa katika Hospitali ya Mkuranga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad