HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 12, 2017

FILBERT BAYI AFUNGA KOZI YA UTAWALA BORA KWA WADAU WA MPIRA WA MIGUU


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

KATIBU mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi amefunga kozi ya utawala bora iliyoendeshwa na mkufunzi wa FIFA Henry Tandau iliyokuw ainafanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam

Kozi hiyo inayosimamiwa na Kamati ya Olimpiki ilianza Mei 08 na kufungwa Mei 12 huku kukiwa na washiriki 15 kutoka klabu mbali mbali za ligi kuu na taasisi za michezo.

Akizungumza wakati wa kufunga kozi hiyo Bayi amesema kuwa hii ni kwa mara ya kwanza kwa wawakilishi kutoka klabu mbalimbali za Ligi Kuu kushiriki katika mafunzo haya ambayo ni muhimu sana kwa maendeleo ya michezo nchini.

Amesema kuwa, ana imani kubwa sana kuwa elimu hii waliyoipata wataenda kuitumia vizuri katika kuziendesha klabu zao na kuzieletea maendeleo kwani msingi mkubwa wa maendeleo ya soka ni kuwa na utawala bora.

"Elimu hii mliyoipata leo nina imani kubwa sana mtaitumia vizuri kwani wengi wenu mnatoka katika klabu za Simba, Yanga na Azam na maendeleo ya mpira wa miguu yanaletwa na utawala bora na wasiende kuweka vyeti ndani bali wanatakiwa kuvitumia kwa ajili ya manufaa ya vizazi vijavyo,"amesema Bayi.

Mkufunzi wa FIFA Henry Tandau amemshukuru Bayi kwa kuweza kukubali kuwa mgeni rasmi kaika mafunzo hayo na kumuahidi kuwa elimu hii waliyoipata wanaimani kuwa washiriki wote wataenda kuelimisha na wengine na kuleta utawala bora kwenye klabu zao.

Mafunzo hayo ya siku 5 yameratibiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini huku ikiwa ni kwa mara ya kwanza tofauti na miaka mingine kufanyika mikoani pia yameweza kuleta tija kwa washiriki kufahamu mambo mbalimbali yanayohusu michezo ikiwemo riadha.

Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi akizungumza wakati wa kufunga kozi wa mafunzo ya utawala bora iliyoendesha na Shirikisho la Mpia wa Miguu (FIFA) kupitia kamati ya Olimpiki iliyoanza Mei 08 mpaka Mei 12 Jijini Dar es salaam.
 Mkufunzi wa FIFA Henry Tandau akizungumza wakati wa kufunga kozi wa mafunzo ya utawala bora iliyoendesha na Shirikisho la Mpia wa Miguu (FIFA) kupitia kamati ya Olimpiki iliyoanza Mei 08 mpaka Mei 12 Jijini Dar es salaam. Kulia ni Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi.
 Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi  akitoa cheti cha mafunzo ya utawala bora kwa Mshiriki kutoka Kituo cha JKM Park Kassim Liogope mafunzo yaliyomaliza leo Jijini Dar es salaam.
 Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi  akitoa cheti cha mafunzo ya utawala bora kwa Mshiriki kutoka klabu ya Yangaa ambaye ni afisa masoko na mratibu wa matawi Omari Kaya mafunzo yaliyomalizaleo Jijini Dar es salaam.
  Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi  akitoa cheti cha mafunzo ya utawala bora kwa Mshiriki kutoka Azam Saad Kawemba ambaye ni Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo mafunzo yaliyomalizika leo Jijini Dar es salaam.
  Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi  akitoa cheti cha mafunzo ya utawala bora kwa Mshiriki kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini Wilfred Kidau katika mafunzo  yaliyomalizika leo Jijini Dar es salaam.
\
  Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi  akitoa cheti cha mafunzo ya utawala bora kwa Mshiriki kutoka Klabu ya Simba Said Tuli ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji wa Simba mafunzo  yaliyomalizika leo Jijini Dar es salaam.
  Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi akitoa cheti cha mafunzo ya utawala bora kwa Mshiriki kutoka bodi ya ligi Fatma Abdala mafunzo yaliyomalizika leo Jijini Dar es salaam.
 Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi  akiw akatika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya utawala bora yaliyomalizika leo Jijini Dar es salaam.Picha na Zainab Nyamka.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad