HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 30 May 2017

EMINA HIP YAJA NAKAMPENI MPYA YA NGUVU YA BINTI

Na  Ashraf Said, Globu ya jamii
Tasisi ya Femina Hip imeanzisha kampeni yake mpya inayokwenda kwa jina la Nguvu ya Binti hili kuweza kumsaidia msichana anapokuwa katika siku zake .

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Lydia Charles amesema kuwa Femina Hip imezindua kampeni ya Nguvu ya Binti ambayo itawakilishwa na wasichana wenye historia,Tabia, na uzoefu tofauti .

“ timu mpya ya nguvu ya binti itakuwa na sauti ya wasichana wote nchini Tanzania , wakichimbua , Kujadili na kujaribu kutatua changamoto na vikwazo mbalimbali kwa pamoja” amesema.

Amesema kuwa wasichana hao watakuwa mawakili kwa mambo ya kijamii, Kiuchumi na kisiasa.

Ameliza kwa kusema kuwa Femina Hip pamoja na wasichana wa kundi hilo wanamini kwamba ni lazima kufanya kazi pamoja , kufunguka na kuzungumza kuhusiana na hedhi ,maumivu wakati wa hedhi , Usafi wa miiko inayousishwa na hedhi kwa kushirikisha walimu , wazazi, walezi na Wanaume pia .
 Mratibuwa programu ya Nguvu ya Binti , Lydia Charles akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya mpango wao wa kuwawezesha wanawake wanapokuwa katika siku zao leo katika ofisi zao  katika eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa Kays Hygien, Sauda Simba akizungumzia kuhusu kampuni  ya Femina  iliyodhamini programu hiyo
Sehemu ya Waandishi wa wakufuatilia mkutano 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad