HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 9, 2017

BENKI YA CBA YAIMWAGIA SHULE YA SING'ISI MSAADA WA SHILINGI MILIONI NNE

Na Pamela Mollel, Arusha 
      Shule ya msingi Sing’isi iliyopo katika wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha iliyokuwa ikikabiliwa  na changamoto ya madarasa kujaa maji imepatiwa msaada wa kiasi cha shilingi Milioni nne na benki ya biashara ya Africa (CBA) kwa ajili ya ukarabati wa baadhi ya madarasa

Akikabidhi hundi katika shule hiyo juzi Mkurugenzi wa CBA Gifti Shoko alisema kuwa lengo la msaada huo ni kusaidia wanafunzi kuondokana na changamoto ya kutoa maji katika madarasa pindi mvua zinaponyesha hali inayosababisha kukosa vipindi viwili hadi vitatu kwa siku

Alisema kuwa msaada huo utumike kama ulivyokusudiwa kuboresha madarasa hayo kwani ubora wa elimu unaletwa na mazingira mazuri ya watoto  kusomea  

‘’Hapa nawaona Marais, mawaziri wa kesho pamoja na wafanyakazi wazuri wa benki yetu hivyo hatuna budi kutuoa msaada huu ikiwa kama mchango wetu wa kuboresha sekta ya elimu na tunawahidi hatutaishia hapa tutaendelea kuwasaidia kadri ya uwezo wetu ‘’

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Faith Mushiro akitoa neno la shukrani alisema kuwa wanafunzi wa darasa la tano na la sita ndiyo hasa walikuwa wakipata hadha hiyo ya kuondoa maji madarasani pindi mvua zinapoanza kunyesha

Aidha alisema kuwa zaidi ya vipindi viwili hadi vitatu vya asubuhi hushindwa kuhudhulia kutokana na changamoto hiyo hivyo kupitia msaada huo wanafunzi watasoma katika vyumba  vya madarasa vizuri tofauti na kipindi cha nyuma 

Awali akisoma Risala mwalimu wa shule hiyo Bw.Simon Mbawala  kwa niaba ya shule hiyo alisema kuwa pamoja na msaada waliopatiwa bado shule inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa makataba ya kuhifadhi vitabu, kuharibika kwa sakafu za madarasa pamoja na kupasuka kwa vioo vya madirisha 

Hata hivyo tunatoa shukrani zetu za dhati kwa mssada huu wa ujenzi wa vyumba vinne ambayo vilikuwa na tatizo la kuvuja kwa maji kutokana na bati zake kuwa chakavu hali iliyokuwa ikiwathiri sana wanafunzi na walimu hasa ikifika wakati wa kufundisha

 Mkurugenzi wa Benki ya biashara ya Africa (CBA) Gifti Shoko akikabidhi hundi ya kiasi cha shilingi Milioni nne kwa Mwalimu mkuu wa Shule ya msingi Sing’isi iliyopo katika wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha juzi Bi.Faith Mushiro kwaajili ya kukarabati madarasa manne ambayo hujaa maji kipindi cha mvua hali ambayoilikuwa ikiwasababishia wanafunzi kukosa vipindi viwili hadi vitatu kwa siku.
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Sing'isi Bi.Faith Mushiro akionyesha sehemu ambayo husababisha maji kujaa ndani ya madarasa pindi mvua inaponyesha, wakatikati ni Mkurugenzi wa Benki ya biashara ya Africa(CBA)Gifti Shoko pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo
 Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi  Sing'isi Bi.Faith Mushiro akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa benki ya CBA mara baada ya kupata msaada wa shilingi Millioni nne kwa ajili ya ukarabati wa madarasa.
 Mkurugenzi wa Benki ya biashara ya Africa(CBA)Gifti Shoko akiangalia baadhi ya vifaa vya umeme ambavyo walitoa msaada kwa shule hiyo
 Wanafunzi wakiimba

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad