HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 25 May 2017

BALOZI SEIF AREJEA ZANZIBAR AKITOKEA JORDAN

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na baadhi ya Mawaziri na Watendaji Wakuu wa Serikali mara alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume akitokea Nchini Jordan kushiriki Mkutanowa Jukwaa la Dunia la Uchumi akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Mauungano wa Tanzanmia Dr. John Pombe Magufuli.
Balozi Seif Kushoto akibadilishana Mawazo na Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika chumba cha Watu Mashuhuri {VIP} Kongwe. Picha na – OMPR – ZNZ.Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewasili Zanzibar akitokea Mjini Amman Nchini Jordan kuhudhuria Jukwaa la Dunia la Uchumi World Economy Forum - WCF} la Siku Tatu litakalohudhuriwa na zaidi ya Wajumbe 2,000 kutoka Nchi 58 Duniani.
Balozi Seif alimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kwenye Jukwaa hilo la Kanda ya Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika lililoshirikisha Viongozi Wakuu wa Nchi, Wafanyabiashara,wamiliki wa Makampunni ya Kimataifa, Wawakilishi wa Taasisi za Kiraia, Mashirikia ya Kimataifa, Wana Habari pamoja naVijana wapatao 2,000.


Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipokewa na baadhi ya Mawaziri, Watendaji Wakuu wa Serikali pamoja naViongozi wa Kisiasa. Katika Mkutano huo wa Jukwaa la Dunia la Uchumi Balozi Seif aliongozana na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Balozi Amina Salum Ali, pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa


Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed.


Katika Mkutano huo wa Jukwaa la Dunia la Uchumi Balozi Seif na Ujumbe wake alishiriki Washa ya Utalii iliyojikita zaidi katika masuala ya Kujenga Uchumi kwa Mataifa yaMashariki ya Kati na yale ya Kanda ya Afrika ili kuona njia gani


zinaweza kutoa fursa za ajira kwa Vijana kwa kutumia Teknolojia ya Kisasa


Mkutano huo wa Jukwaa la Uchumi Duniani ulifunguliwa na Kiongozi wa Jordan Mfalme wa Pili Abdullah Bin Al-Hussein kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa King Hussein Bin Talal katika Bahari Nyeusi.Jukwaa la Uchumi la Dunia { World Economy Fforum - WCF} limeasisiwa Mwaka 1971 chini ya Muanzilishi na Mwenyekiti wake Profesa Klaus Schwab huko Davos, Switzerland.


Othman Khamis Ame

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

24/5/2017.
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad