HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 25 May 2017

ALIYEBUNI NEMBO YA TAIFA AHAMISHIWA MUHIMBILI KWA MATIBABU

  Mzee Francis Maige Ngosha (kwenye kitanda) akitolewa katika Hospitali ya Rufaa Amana tayari kwa kupelekwa Hosptali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.

Na Anthony John Globu ya Jamii.
Serikali imeahidi kumpatia matibabu Mzee Francis Ngosha  aliyebuni Nembo  ya taifa. Hatua hiyo imekuja baada ya kituo cha Runinga cha ITV  Dar es salaam kumuonesha mzee huyo akiwa katika hali mbaya katika eneo Buguruni ambapo alikutwa akiishi kwenye chumba kimoja alichopewa  na msamaria mwema.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo hii katika hospitali ya Rufaa ya Amana  DKT, Hamisi Kigwangalla amesema mchango wamzee huyu ni mkubwa ambao utakumbuka na vizazi vyote nchini kwa suala hilo alilolifanya.
Aidha  Kigwangalla amesema kuwa  serikali ilipata tarifa juu ya madhira  anayoyapata hivyo serikali ilimuagiza kuchukua hatua za haraka  za kumsaidia mzee huyu.
‘’Katika hatua hii tunashughulika na  suala matibabu na baada ya matibabu kukamilika tutamtafutia makazi ya kuishi kama atakubali atapelekwa katika nyumba ya wazee wasiojiweza iliyopo Nunge au tumtafutie nyumba kwaajili ya kuishi’’amesema Kigwangalla.
 Mzee Francis Maige Ngosha (kwenye kitanda) akiwa kwenye gari la wagonjwa tayari kwa kupelekwa Hosptali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi. (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii).
  Naibu Waziri,Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Hamisi Kigwangalla akimjulia hali Mzee Francis Maige Ngosha aliyelazwa kwenye wodi ya Wanaume Hospitali ya Rufaa Amana leo jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri Dk. Hamisi Kigwagalla akiongea na waandishi wa habari kuhusu hatua waliyochukua ya kumuhamishia Mzee Maige kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Kitengo cha Dharura Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Juma Mfinanga akizungumza na Mzee Francis Maige mara baada ya kupakiwa kwenye gari ya kubeba wagonjwa tayari kwa kupelekwa Muhimbili leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad