HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 24, 2017

YANGA YAWAPA KONGOLE WACHEZAJI, YAZINDUA MCHAKATO WA WANACHAMA KUCHANGIA TIMU



Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa akizungumza na waandishi wa habari.

Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

UONGOZI wa klabu ya Yanga umetoa pongezi kwa wachezaji wa timu hiyo kwa kuweza kutinga hatua ya nusu fainali kombe la ASFC baada ya kuibanjua Tanzania Prisons goli 3-0 mchezo uliopigwa jumamosi katika dimba la Taifa. 

Yanga imefanikiwa kuingia hatua hiyo na tayari amegusia maandalizi ya timu kuelekea mchezo wa nusu fainali ASFC tarehe 30 April dhidi ya Mbao FC jijini Mwanza . 

Droo ya nusu fainali ASFC ilifanyika jana jioni . Mabingwa hawa watetezi Yanga SC watawavaa Mbao FC na Simba SC watakwaana na Azam FC uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam tarehe 29 April 2017.

Katibu Mkuu Charles Boniface Mkwasa amesema kuwa wanaheshimu uwezo wa Mbao na wao wanajipanga vyema kupata ushindi katika uwanja wa Kirumba . Benchi la ufundi baada ya droo ya jana na kujua mpinzani wetu ni nani , tayari wameanza mazoezi kujiandaa na mchezo huo .

Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Mkwasa ametumia mkutano huo kueleza hatua ambayo klabu imechukua katika kuongeza mapato ya klabu hiyo kutokana na kulegalega kwa hali ya uchumi klabuni hapo . 

Hatua iliyochukuliwa ni kufungua akaunti maalumu ambayo itawapa fursa wapenzi , wanachama, mashabiki na wadau wa timu hiyo kuichangia fedha klabu yao ili kuipa nguvu ya misuli ya kiuchumi. 

"ni ombi la wanachama wenyewe kujitolewa kuichangia timu yao na sisi kama uongozi tumeona ni jambo lenye tija . Hii haina tafsiri ya kwamba klabu haina fedha na imekwama kabisa kujiendesha bali tumelipitisha ili kukidhi matakwa ya wengi," alisema Mkwasa. 

Mkwasa alisema kuwa anafahamu wote wanaokuja uwanjani au kulipia kadi kama sehemu ya kuongeza mapato ya klabu lakini kwa mfumo huu ambao tunaenda kuuzindua utatoa fursa kwa kila mdau popote alipo kuichangia klabu kama sehemu ya kujivunia timu hii na kusimama kama nguzo muhimu ya maendeleo ya klabu.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad