HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 11 April 2017

YANGA WATOA TAMKO JUU YA KAMATI YA SAA 72, YAIONYA KUTENDA HAKI RUFAA YA SIMBA

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Yanga Salum Mkemi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tamkom lao juu ya maamuzi na utendaji wa kmati ya saa 72 dhidi ya rufaa ya timu ya Simba dhidi ya Kagera. Kushoto ni Katibu  Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

WAJUMBE wa kamati ya Utendaji wa Yanga wameweka wazi maamuzi yao ya kutakuwa na imani na maamuzi na utendaji wa kamati ya saa 72 kwa rufaa mbalimbali zilizowakilishwa wao kubwa ikiwa rufaa ya Simba SC kwa Kagera Sugar.

Viongozi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Yanga Mhandisi Paul Malume , wamesema hawana imani na kamati hiyo na kinachoendelea ni kutaka kuvuruga utulivu wa ligi kuu na soka kiujumla .

Mjumbe wa kamati ya Utendaji Salumu Mkemi mjumbe kamati kuu Yanga SC amesema kamati hiyo haina usawa pia ni kamati inayoundwa na zaidi ya wanachama 6 wandamizi wa Simba SC na wao kama Yanga wakiwa na wanachama wawili tu.

Mkemi amesema kuwa tayari wameziangazia harufu na fununu ya kubadilishwa kwa ripoti za michezo ambayo Simba wanasema mlinzi wa Kagera Mohamedi Fakhi alipata kadi 3 za njano .

" kamati hii imechelewa kutoa maamuzi kwa kuandaa ripoti za uongo za michezo dhidi ya Fakhi pia tuna taarifa za kughushiwa email na nyaraka zingine ili kuipa alama tatu Simba SC yenye zaidi ya wajumbe 6 katika kamati hiyo sisi kama Yanga tumeanza uchunguzi wetu na kutoa taarifa kwa vyombo husika vya dola pia maamuzi yoyote ya kuibeba Simba tutakwenda mahakamani licha ya sheria za FIFA kukataza hivyo kama hawataki tufike huko lazima haki itendeke. .." alieleza mjumbe huyo.

Mkemi amesema kuwa tayari wameshavijulisha vyombo husika yaani Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na watu wa makosa ya mtandao (cyber crime) na Mamlaka ya mawasiliano Nchini (TCRA)  juu ya uchunguzi wa mawasilano ya waamuzi wote waliosika na kutajwa kwenye rufaa hiyo.

" tuache kumtafuta bingwa wa mezani na sisi tumefungwa karibu mechi tatu na hatujalilia alama za mezani kwanini wao,  mbona jana wamecheza mchezo mzuri mwishoni na kupata ushindi wa jioni dhidi ya Mbao na hakuna kelele tena na tunawapongeza kwa come back ile . Hiki ndicho mashabiki wa timu hizi wanakitaka . Ushindi wa uwanjani sio figisu . "

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Yanga Salum Mkemi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tamkom lao juu ya maamuzi na utendaji wa kmati ya saa 72 dhidi ya rufaa ya timu ya Simba dhidi ya Kagera. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Yanga, Siza Lyimo, shoto ni Katibu  Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa na Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Yanga Mhandisi Paul Malume .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad