HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 12, 2017

YANGA KUODOKA NA MSAFARA WA WACHEZAJI 20 KESHO, CHIRWA ABAKI

Katibu Mkuu wa Yanga Chrles Mkwasa.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Kelekea mechi ya marudiano ya mchezo wa hatua ya mtoano wa Kombe la Shirikisho baina ya wawakilishi wa Tanzania  klabu ya soka ya Yanga na Mc Alger ya Algeria imeweka wazi kikosi cha wachezaji 20 watakaoondoka kesho kueleo nchini Algeria kesho jioni.

Yanga wanatarajiw akuondoka kesho majira ya saa 12 jioni kuelekea nchini Algeria ambapo watacheza na MC Alger siku ya Jumamosi katika Jiji la Alger.

Akiweka kikosi hicho , Katibu Mkuu wa Yanga Chrles Mkwasa amesema kuwa tayari wachezaji wapo tayari kwa ajili ya kwenda kupambana nchini Algeria na tunafahamu ni mchezso mgumu lakini pia ni muhimu sana kwao wakihitaji ushindi wa aina yoyote au sare ili kusonga mbele na kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.

Mkwasa amesema kuwa anapenda kuwa msafara wa wachezaji 20, benchi la ufundi na viongozi utaondoka kesho jioni majira ya saa 12 kwa ndege ya shirika la Emirate kupitia Dubai.

Wachezaji watakaondoka ni Makipa; Deogratius Munishi na Beno Kakolanya . Nafasi ya ulinzi ni ; Nadir Haroub , Vicent Bossou , Juma Abdul , Vicent Andrew, Oscar Joshua , Juma Abdul , Mwinyi Haji, Hassan Kessy na Kelvin Yondani. 

Nafasi ya viungo ni; Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deusi Kaseke,Said Makapu, Juma Mahadhi, Saimoni Msuva, Geofrey Mwashuiya na Emmanuel Martin.
 Upande wa washambuliaji ni Amissi Tambwe na Donald Ngoma

Wachezaji wafuatao wataukosa mchezo huo kwa sababu mbalimbali Justine Zulu,Malimi Busungu,Matheo Antony,Ally Mustapha,Pato Ngonyani ,Obrey Chirwa na Yusuph Mhilu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad