HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 24 April 2017

WAZIRI SIMBACHAWENE AZINDUA TAWI LA DCB MKOA WA DODOMA LEO.


Waziri wa Nchi ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. George Simbachawene (MB) ameipongeza benki ya DCB kwa hatua kubwa waliyofikia ya  kwa kuwa miongoni mwa benki zilizoanzisha huduma zinazoendana na teknolojia ya kisasa kama ilivyo kwa huduma za kibenki kwa njia ya mawakala (DCB Jirani) na huduma za kibenki kwa njia ya simu za mkononi (DCB Pesa).

Simbachawene amesema kufunguliwa kwa tawi hili zitasogeza huduma za kibenki karibu na wafanyabishara na wakazi wa mji wa Dodoma na haya ndiyo maendeleo tunayotaka katika sekta ya kibenki ili huduma za benki zipatikane kwa urahisi zaidi kwa wananchi na nina hakika wananchi wengi watapata huduma bora kupitia tawi hili. 
Hivyo nawaasa wafanyabiashara, wafanyakazi na wakazi wote wa mkoani Dodoma watumie fursa hii kwa kufungua akaunti mbalimbali za DCB kupitia tawi hili, ni imani yangu kwamba huduma zitakozotolewa na tawi hili zitakuwa bora na zenye kumjali mteja.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB Edmund Mkwawa ametoa shukrani za dhati kwa Mhe. George Simbachawene, Waziri wa TAMISEMI kwa kukubali kuwa Mgeni rasmi katika hafla hii ikiwa ni mara yako ya pili kukubali wito kuwa mgeni rasmi. Mara ya kwanza ilikuwa ni kuzindua rasmi tawi la Benjamini Mkapa lililopo maeneo ya Samora karibu na ofisi za Halmshauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Mkwawa amesema kwa upande wa Dodoma wamefanikiwa kupata mawakala 38 ambao muda si mrefu wataanza kutoa huduma za DCB mitaa ya Dodoma karibu zaidi na wananchi. Mbali na hapa Dodoma, pia wana mpango wa kupeleka huduma za DCB mikoa mingine kupitia DCB Jirani kama vile mikoa ya Pwani, Morogoro, Tanga, Mwanza, Geita, Shinyanga, Kahama, Mtwara, Arusha, Iringa na Mbeya lengo ni kuwa na mawakala 1,500 nchi nzima kufikia Disemba mwaka huu. 

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya DCB Prof . Lucian Msambichaka  ametoa wito kwa wakazi wote wa Dodoma na vitongoji jirani wazipokee huduma za DCB na wawe mstari wa mbele kutumia huduma za benki tawini hapo ili kukuza tawi hili na kuwa na uwezo mkubwa wa kuwahudumia wananchi wengi zaidi katika suala zima la kupiga vita umasikini. 

Prof Msambichaka ameongezea na kusema wana imani wengi watanufaika na benki hii kwa kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba mara kwa mara, kuimarisha usalama wa fedha zenu na kujenga uwezo wa kupanua biashara kwa kutegemea. Huduma hizi zina lengo la kusogeza huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi na kuongeza amana za benki ambazo ndio uti wa mgongo wa benki zote duniani.
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. George Simbachawene (MB) akizundua tawi la Benki ya DCB mkoa wa Dodoma akishuhudiwa na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania John Malecela(Kulia) Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB Edmund Mkwawa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya DCB Prof . Lucian Msambichaka .

Mgeni rasmi Waziri wa Nchi ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. George Simbachawene (MB) akizungumza kabla ya uzinduzi wa tawi jipya la Benki ya DCB mkoa Dodoma na kuwapongeza kwa hatia kubwa waliyofikia ya kuendelea kutanua huduma zao nje ya Mkoa wa Dar es salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB Edmund Mkwawa (kushoto) akisalimiana na Mgeni rasmi Waziri wa Nchi ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. George Simbachawene (MB) wakati akiwasili jengo la LAPF Mkoa wa Dodoma wakati wa uzinduzi wa tawi la DCB mkoani humo. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya DCB Prof . Lucian Msambichaka

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania John Malecela akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi la Benki ya DCB Mkoa wa Dodoma na kuipongeza hatua kubwa waliyoifanya ya kutanua huduma mpaka mikoani na kuwataka waendelee kufikiria na mikoa mingine. Ufunguzi huo umefanyika leo Mkoa wa Dodoma.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya DCB Prof . Lucian Msambichaka akizungumzia namna benki ya DCB ilivyoweza kujiendeleza kwa kipindi cha miaka 15 na hatua kubwa waliyoifikia ya kufungua tawi Mkoa wa Dodoma.

Meneja wa matawi ya Benki ya DCB mkoa wa Dar es salaam wakiwa wameenda kushuhudia uzinduzi wa tawi la benki hiyo Mkoa wa Dodoma uliofanyika leo.

Wafanyakazi wa Benki ya DCB mkoa wa Dodoma wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa tawi la benki hiyo leo Mkoani Dodoma.

Kikundi cha Ngoma kutoka Mkoani Dodoma kikitumbuiza katika hafla ya uzinduzi wa tawi la Benki ya DCB Mkoa wa Dodoma uliofanyika leo.

Wageni mbalimbali wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Tawi la Benki ya DCB leo Mkoani Dodoma.

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania John Malecela akisaini katika kitabu cha wageni wa uzinduzi wa  Tawi la Benki ya DCB leo Mkoani Dodoma. Picha na Geofrey Adorph, Dodoma

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad