HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 21, 2017

WAZIRI MKUU AUNGANA NA WABUNGE KUUAGA MWILI WA DKT. ELLY

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameungana na wabunge katika kuuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Dkt. Elly Macha aliyefariki Machi, 31, 2017 katika hospitali ya New Cross Wolverhampton nchini Uingereza.
Akizungumza katika tukio hilo Waziri Mkuu ametoa pole kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai, familia marehemu pamoja na wabunge wote.
Waziri Mkuu amesema enzi ya uhai wake marehemu Dkt. Elly alitoa mchango mkubwa na ushauri mzuri katika masuala ya elimu na uboreshaji wa maeneo ya watu wenye ulemavu.
Awali akisoma wasifu wa marehemu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mheshimiwa Mchungaji Peter Msigwa alisema Dkt. Elly alipata ulemavu wa macho akiwa na umri wa miezi mitano baada ya kuugua ugonjwa wa surua.
Mchungaji Msigwa alisema pamoja na kuwa na ulemavu huo wa macho lakini haukuwahi kuwa kikwazo kwake kwani aliweza kufanya jambo lolote lililokuwa ndani ya uwezo wake.
Mwili wa marehemu Dkt. Elly umesafirishwa leo kwenda nyumbani kwake Usa River mkoani Arusha na anatarajiwa kuzikwa kesho nyumbani kwa wazazi wake katika kijiji cha Kirua Vunjo mkoani Kilimanjaro.
Dkt. Elly alizaliwa Juni 18, 1962 kwenye kijiji cha Kirua Vunjo mkoani Kilimanjaro, ambapo mbali na wadhifa wa ubunge pia  aliwahi kuwa Mshauri Mwelekezi wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu vya Afrika Mashariki.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (Kulia), Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (wa pili kulia) wakishuhudia mwili wa Marehemu Mhe. Elly Macha ukiwasili, Marehemu aliefariki Mwezi uliopita katika Hospitali ya New Cross, Wolverhampton, nchini Uingereza  baada ya mwili kuwasili  leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa heshima za Mwisho katika jeneza la Marehemu Mheshimiwa Dr Elly Marko Macha Mbunge wa Viti maalumu Chadema ambaye mwili wake ulifikishwa katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma kwa ajili ya Bunge kuaga mwili wa Marehemu Dr Macha alifariki akiwa katika matibabu Nchini Uingereza.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza  wakati wa kuagwa kwa  mwili wa Mhe. Elly Macha aliefariki Mwezi uliopita katika Hospitali ya New Cross, Wolverhampton nchini Uingereza na mwili wake umeagwa  leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa salamu za Serekali katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma wakati wa shughuli ya kuaga Mwili wa Maerehemu Mheshimiwa Dr Elly Marko Macha ambaye alifariki Nchini Uingereza alipokuwa katika matibabu
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiaga mwili wa marehemu Mhe. Elly Macha aliefariki Mwezi uliopita katika Hospitali ya New Cross, Wolverhampton, nchini Uingereza na mwili umeagwa  leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiaga mwili wa marehemu Mhe. Elly Macha aliefariki Mwezi uliopita katika Hospitali ya New Cross,Wolverhampton nchini Uingereza na mwili wake umeagwa leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe, Kassim Majaliwa wakati wa kuagwa kwa mwili wa Mhe. Elly Macha aliefariki Mwezi uliopita katika Hospitali ya New Cross, Wolverhampton nchini Uingereza na mwili wake umeagwa leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa mkono wa pole Glory Haika Peter (24) ambaye ni Mtoto wa Maerehemu Mheshimiwa Dr Ell Macha Mbunge viti Maalumu Chadema ,Wakati wakusindikiza Mwili wa marehemu katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad