HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 19, 2017

WATUHUMIWA 267 WAKAMATWA JIJINI DAR ES SALAAM KWA MAKOSA MBALIMBALI.

 Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam Simon Sirro akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na watuhumiwa waliokamatwa kwa Makosa mbalimbali ya kiharifu katika jiji la Dar es Salaam.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam Simon Sirro akionyesha baadhi ya vitu mbalimbali walivyo vikamata leo alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari.

Na Ripotawetu Globu ya Jamii
Jeshi la Polisi limewakamata Jumla ya watuhumiwa 267 kwa Makosa mbalimbali ya kihalifu pamoja na Madawa ya kulevya, Unyang'anyi wa kutumia Silaha katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda Polisi kanda Maalum Dar es salaam Simon Sirro amesema operation hii ni endelevu na jumla ya kete 366 za dawa za kulevya zimekatwa pamoja  puli za bangi 150 na Misokoto ya bhangi 51.

Aidha Sirro amesema kuwa Operatini kali ya kuwasaka wahalifu wa makosa hayo mbalimbali ikiwemo kosa la kupatikana na madawa ya kulevya  bado inaendelea na hivyo tunawaomba raia wema waendelee kutoa Ushirikiano mzuri kwa Jeshi la Polisi ili kufanikisha kukamatwa kwa waalifu.

" Watuhumiwa wote kwa ujumla bado wanaendelea kuhojiwa kulingana na makosa yao na pindi  upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kwa hatua nyingine zaidi" amesema Sirro.

Pia Kamishna huyo ameongeza kuwa mnamo tarehe 15 mwezi huu 2017 majira ya saa moja usiku maeneo ya Kiwalani kwa Ally Mboa, Jeshi la polisi limefanikiwa kukamata silaha moja aina ya Shotgun ambayo imekatwa kitako na mitutu na huku namba zake zikiwa zimefutwa.

" Siraha hiyo ilipatikana wakati Askari wakiwa doria katika maeneo hayo ambapo yaliskia harufu ya bhangi na kuanza kufuatilia ili kubaini ilipokuwa ikitokea. Ghafla watu wawili wasiofahamika walikurupuka na kupanda pikipiki ambayo haikusomeka namba kisha kuangusha begi moja la mgongoni ambalo lilikuwa na Silaha" amesema Sirro.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad