HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 12 April 2017

WANAODAIWA KUWA MAJAMBAZI WALIOFANYA MATUKIO YA UHALIFU SINZA NA BOKO WAFARIKI, ASKARI FEKI ANASWA

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikiria  watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi ambao walifanya matukio mawili tofauti ya uporaji katika maeneo ya Boko pamoja na Sinza jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam , Kamishina Simon Sirro amesema majambazi waliwanasa wakiwa katika uhalifu wa uporaji baadhi ya maduka ya Boko.
Kamishina Sirro amesema wakati polisi  wakiwa katika operesheni walifika maeneo hayo kisha majambazi wakaanza kutupa  risasi na polisi wakajibu na kuwapiga na wakaanguka ndipo waliweza kuwachukua kwa ajili ya matibabu katika hospitali ya Taifa Muhimbili  ambapo walifariki wakiwa wanapatiwa matibabu.
Wakati huo huo jeshi la polisi limewakamta watu wawili ambao walikuwa wanazalisha Konyagi bandia ya chupa. Watuhumiwa hao ni Bahati Steve pamoja na Vumilia Andrea na uchunguzi unaendelea dhidi yao.
Hata hivyo jeshi la polisi limeweza kukamata dawa za kulevya mbalimbali  pamoja na pombe zilizo katika vifungashio vya plastiki (Viroba).
Pia Jeshi la Polisi limeweza kumnasa Askari Feki  Lyanga Baruti ambaye amesema sare za jeshi hilo aliziiba kwa kaka yake na kasha kuvaa.
Baruti amesema alizivaa na kwenda sehemu mbalimbali na kisha askari wakaweza kumnasa akiwa katika mizunguko yake.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam , Kamishina Simon Sirro akizungumza na waandishi habari juu ya operesheni ya wiki moja iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam , Kamishina Simon Sirro akionyesha konyangi bandia walizozikamata katika operesheni leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi  Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro  akimuonyesha Askari Feki, Lyanga Baruti mbele ya waandishi habari juu ya jinsi alivyoiba sare za polisi za kaka yake na kuanza kukata mitaa katika jiji Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam , Kamishina Simon Sirro akionyesha magazine na risasi walizozikuta kwa majambazi waliofanya matukio ya ujambazi kwa wiki ya iliyopita.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam , Kamishina Simon Sirro akionyesha magari ya ambayo yameibiwa kwa watu leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad