HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 22 April 2017

WANACHAMA WA CUF WAZIPIGA 'KAVU KAVU' KATIKA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI DAR LEO

Wanachama wa chama cha Wananchi CUF wakionyeshana umwamba baada mvurugano kutokea katika makundi mawili (lile linalomuumnga mkono Prof. Lipumba na linalomuunga mkono Maalim Seif) baada ya kundi moja wapo kudaiwa kuvamia mkutano wao na waandishi wa habari uliokuwa ukifanyika katika Hotel ya Vinna, Mburahati jijini Dar es salaam.

Baada ya kufanikiwa kuvuruga mkutano huo baadhi ya watu waliokuja kufanya vurugu wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa kundi moja wapo walikimbia na wengine kudhibitiwa na wananchi wenye hasira. haikufahamika kwa haraka sababu za watu hao kuvamia na kuuzuia mkutano huo.
Timbwili likiendelea na kupelekea bwana huyu kushoto akichezeshewa kichapo.
mara uzalendo ukamshinda akasalimu amri na kukaa chini baada ya kudhibitiwa na wananchi.
 Mtu huyo anaedaiwa kutoka kambi nyingine ya Chama hicho akiugulia maumivu baada ya kuumia katika mtafaruku huo.
Mambo yalivyoanza kabla ya mpambano kuanza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad