HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 19, 2017

UHAMIAJI WAFANYA UZINDUZI WA MFUMO WA KUHAKIKI VIBALI VYA UKAAZI KI - ELEKTRONIKI



  Kamishna Jenerali  wa Idara ya Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akifafanua jambo kwa  waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa kielektroniki wa uhakiki  vibali vya ukaazi ujulikanao kama  “E – Verification” mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
 Kamishna Jenerali  wa Idara ya Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (kulia) akizungumza na maafisa Uhamiaji na  waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa kielektroniki wa uhakiki vibali vya ukaazi ujulikanao kama  “E – Verification” mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya maafisa Uhamiaji na waandishi wa habari wakimsikiliza Kamishna Jenerali  wa Idara ya Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa kielektroniki wa uhakiki  vibali vya ukaazi ujulikanao kama  “E – Verification” mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Afisa TEHAMA, Mkaguzi wa Uhamiaji Sokolo Kaseko akifafanua na kuelekeza mbele ya Waandishi wa Habari jinsi ya kufanya Uhakiki wa Vibali Ki- elektroniki wakati wakati wa Uzinduzi wa Mfumo Uhakiki wa Vibali vya Ukaazi ki-elektroniki uliofanyika Ukumbi wa Mikutano, Makao Makuu ya Uhamiaji, Dar es Salaam.
 Kamishna Jenerali  wa Idara ya Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (kulia) akifuatilia jambo wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa kielektroniki wa uhakiki vibali vya ukaazi ujulikanao kama  “E – Verification” mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Afisa Utawala na Fedha wa Uhamiaji Edward Chegero na kushoto ni Afisa wa vibali na Pasi wa Uhamiaji Musanga Etimba.

Frank Mvungi-Maelezo
Serikali imezindua mfumo wa Kielektroniki wa Uhakiki  wa Vibali vya ukazi “e-verification” hapa nchini ili kuongeza tija na kudhibiti upotevu wa mapato.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mfumo huo.
Akizungumzia mfumo huo Kamishna Jenerali Makakala amesema utasaidia Makampuni, Taasisi,  Mashirika na watu binafsi kuhakiki vibali vya watumishi wao ili kuona kama ni halali ama  si halali na idara hiyo itakuwa tayari kuwasaidia wale wote watakaokuwa na matatizo kupata ufumbuzi wa changamoto zao.
“Idara inatoa siku 90 kwa watu wote kuhakiki vibali vyao vya ukazi ili kama wana matatizo wasaidiwe kupata ufumbuzi” Alisisitiza Dkt Makakala.
Akizungumzia lengo la mfumo huo Makalala amesema utasaidia kuimarisha udhibiti wa wageni wanaoishi hapa nchini na kuzuia mianya ya upotevu wa maduhuli ya Serikali na mfumo huo ni rahisi na unatoa fursa kwa wageni wote wenye vibali vya ukaazi kuhakikiki kumbukumbu za vibali vyao ili kujua kama vimetolewa na Idara hiyo.
Aidha,Idara ya Uhamiaji inawaomba wadau wa huduma zake kufika wao wenyewe katika Ofisi zao katika  ngazi ya Wilaya, Mikoa na Makao Makuu kwani huduma za Uhamiaji hazina uwakala.
Mfumo huo wa uhakiki wa vibali vya ukaazi kwa kutumia njia ya kielektroniki “e-verification” unapatikana kupitia tovuti ya uhamiaji ya www.immigration.go.tz.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad