HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 27, 2017

TSSA YATEMBELEA KIWANDA CHA NYAMA MJINI SHINYANGA

Jumuiya ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini kupitia (TSSA) inayoundwa na Mifuko ya NSSF, PPF, LAPF, PSPF, GEPF, NHIF, WCF pamoja na ZSSF imefanya ziara ya kutembelea kiwanda cha nyama kilichopo mjini Shinyanga ambacho hakikuwahi kufanya uzalishaji tangu kibinafisishwe, lengo la Ziara hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kuona hali halisi ya kiwanda hicho ambacho kwa sasa kipo chini ya mikono ya Serikali, Mifuko hiyo kwa pamoja kupitia umoja wao wa TSSA wamedhamiria kuwekeza kwa pamoja katika sekta ya ngozi, nyama na nguo katika kiwanga hivyo. wanaonekana mbele ni  Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa GEPF, Daud Msangi (wa pili kulia).
Wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini kupitia Jumuiya yake ya TSSA (Tanzania Social Security Association) wakipatiwa maelezo wakati walipotembelea kiwanda cha nyama kilichopo mjini Shinyanga, ambacho hakikuwahi kufanya uzalishaji tangu kibinafisishwe. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa GEPF, Daud Msangi akisaini kitabu wakati walipotembelea kiwanda cha nyama kilichopo mjini Shinyanga, ambacho hakikuwahi kufanya uzalishaji tangu kibinafisishwe. Kulia ni Mratibu wa ziara hiyo kutoka TSSA, Meshack Bandawe.
Wakikiangalia maeneo mbalimbali ya usindikaji Nyama.
Wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini kupitia Jumuiya yake ya TSSA (Tanzania Social Security Association) wakiendelea na ziara yao katika kiwanda cha nyama kilichopo mjini Shinyanga.
Sehemu ya Majengo ya kiwanda hicho.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad