HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 28 April 2017

TEACHER’S JUNCTION YATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI KATIKA MTIHANI WA UJIRANI MWEMA

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
TEACHER’S Junction imetoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri mtihani wa ujirani mwema kwa shule 19 binafsi.

Akizungumza katika hafla hiyo Mwalimu Mstaafu na aliyekuwa Mmiliki wa Shule Binafsi, Athuman Ahmed amesema kuwa mashindano upimaji wa wanafunzi kwa mtihani kutaongeza taaluma kwa wanafunzi hao.

Ahmed amesema kuwa Teacher’s Junction wamekuwa kiungo kwa shule za sekta binafsi katika kuratibu masuala ya mitihani ya ujirani mwema.

Amesema kuwa wanafunzi walioshinda wameonesha uwezo wao na wakiendelea watakuwa ni hazina kwa taifa.

Afisa Miradi wa Teacher’s Junction, Salum Njama amesema kuwa wataendelea kuwa na mitihani mbalimbali katika kuwaandaa wanafunzi kitaaluma na sio ushindani kwa shule.

Njama amesema shule zilizoshiriki katika mtihani huo 19 ambapo wanatarajia ushiriki wa shule nyingi na kuweza kujua viwango vya taaluma kwa wanafunzi.

Amesema wamefanya katika Mikoa ya Arusha , Mbeya pamoja na Mwanza na kila sehemu iliyofanyika wanafunzi wameonyesha uwezo kitaaluma.


Mwalimu Mstaafu, Athuman Ahemed akizungumza wakati wa utoaji zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri mtihani wa ujirani mwema ulioratibiwa na Teachers’s Junction kwa shule binafsi leo jijini Dar es Salaam.


Afisa Miradi wa Teacher’s Junction, Salumu Njama akizungumza juu ya uandaaji wa mtihani wa ujirani mwema kwa shule binafsi wakati utoaji zawadi kwa wanafunzi iliofanyika leo jijini Dar es Salaam.


Walimu, wanafunzi pamoja na Teacher’s Junction wakiwa katika picha ya pamoja baada ya hafla ya utoaji zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad