HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 18 April 2017

SERIKALI INAWEKA MAZINGIRA BORA YA KUFANYIA BIASHARA –PROFESA MKENDA

Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda amesema serikali inaweka mazingira  bora kwa wafanyabiashara ili waweze kuendelea katika kujenga uchumi.
Profesa Mkenda ameyasema hayo wakati  wa mkutano wa  mfuko wa sekta binafsi nchini (TPSF), Mkenda amesema sekta binafsi inahitajika katika sekta ya viwanda ili nchi iweze kufikia uchumi wa kati ikiwa ni pamoja na kuongeza ajira kwa vijana.
Amesema kuwa masuala yote ambayo yanayohusu yaingizwe katika kamati iliyoundwa ili kuweza kufanyiwa kazi kwa maandishi juu mazingira ya sekta binafsi kufanya biashara na nchi ipate maendeleo.
Mkenda  amesema kuwa serikali inafanya jitihada kila namna ya jinsi  kuwawezesha  wafanyabiasha kuendesha biashara zao  na changamoto ziwekwe katika maandishi katika kuzifanyia kazi pamoja na kushauri.
Kwa upande  wa wafanyabiashara wamesema mamlaka za udhibiti zinafanya kazi kama biashara wakati  kazi zao ni za utoaji wa huduma.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Alaska Tanzania,  Jennifer Bash amesema watendaji wawasaidie wafanyabiashara katika kupata huduma mbalimbali ili Tanzania iweze  kukua kiuchumi kupita sekta binafsi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda akizungumza katika mkutano wa sekta binafsi kujadili masuala mbalimbali ya biashara nchini leo jijini  Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Sekta Binafsi nchini  (TPSF), Dk. Reginald Mengi akizungumza katika mkutano kujadili masuala ya biashara nchini leo.


Mjumbe wa bodi ya TPSF, Silvester Koka akichangia maada katika Mkutano wa sekta binafsi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Alaska Tanzania, Jennifer  Bash  akichangia maada katika Mkutano wa sekata binafsi nchini leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad