HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 10 April 2017

ROMA MKATOLIKI AZUNGUMZIA SAKATA LA KUTEKWA KWAKE NA WASANII WENZAKE, AONGOZANA NA WAZIRI MWAKYEMBE

Msanii wa bongo Fleva kutoka Tanzania Ibrahim Musa aka Roma Mkatoliki akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jioni hii wakati akizungumzia sakata la kutekwa kwake pamoja na wasanii wenzake katika studio ya Tongwe Records iliyopo Masaki jijini Dar es salaam, Roma ameiomba serikali kuwahakikishia ulinzi wasanii pamoja na watanzania kwa ujumla kwakuwa inaonesha hawana usalama kabisa kutokana na tukio lenyewe lilivyowatokea , kushoto ni Waziri wa habari , Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe.


 

Roma Mkatoliki akifafanua zaidi kwa waandishi wa Habari kwa namna alivyotendewa na hao waliowateka.

Roma akiwaonesha wana habari namna alivyojeruhiwa na waliokuwa akiteswa na hao watekaji ambao mpaka sasa hawajajulikana ni akina nani,kufuatia Uchunguzi/upepelezi wa tukio hilo ukiendelea.
Waziri wa habari , Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe akimsikiliza kulia Msanii wa bongo Fleva kutoka Tanzania Ibrahim Musa aka Roma Mkatoliki akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jioni hii wakati akizungumzia sakata la kutekwa kwake paoja na wasanii wenzake katika studio ya Tongwe iliyopo Masaki jijini Dar es salaam, Roma ameiomba serikali kuwahakikishia ulinzi wasanii pamoja na watanzania kwa ujula kwakuwa inaoyesha hawana usalama kabisa kutokana na tukio lenyewe lilivyowatokea , kushoto ni Mkewa wa Msanii huyo Bi Nancy.
PICHA NA MICHUZI JR

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad