HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 27, 2017

RC GAMBO AZINDUA BARABARA ARUSHA,AKAGUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO , SAMBAMBA NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI KUSIKILIZA KERO ZAO

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gamboa akiwa ameshika mkasi ishara ya kukata utepe katika uzunduzi wa barabara ya St.James na Mahakamani leo Jijini Arusha,Kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqarro.Picha na Vero Ignatus Blog.
Watoto wenye ulemavu kutoka shule ya msingi Meru wakiimba wimbo wa Taifa kama picha hapo juu inavyoonekana wakiongozwa na mwalimu Neema Lema ,na hii inayofuata hapa chini wakiongozwa na mtafsiri na mwalimu Viola Wilson.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha akiangalia kwa makini kile ambacho mtoto mwenye ulemavu Amina kutoka shule ya msingi Meru akitumia kompyuta katika kuhariri video aliyoichagua,aliyeshika kipazasauti ni mtaalam wa masomo ya Tehama katika kitengo cha walemavu bi.Betha Denis.Picha na Vero Ignatus Blog.
 

Na.Vero Ignatus ,Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amtembelea na kujionea mradi wa darasa la watoto wenye ulemavu  katika shule ya msingi Meru iliyopo Jijini hapa. 

Akiwa katika shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 68 miongoni mwao wasichana wakiwa 34 na wavulana 28 huku walimu viziwi wakiwa wawili na mtaalam mmoja wa kitengo cha I. C. T, Gambo alijionea mwenyewe jinsi wanafunzi hao wanavyofanya kazi kwa kutumia teknolojia hiyo. 

Akisoma risala mbele ya Mkuu huyo wa mkoa  mwalimu Musa Lwambano alisema shule hiyo unajumla ya walimu 42 ambapo walimu 15 ni wa kitengo na 27 wa shule ya kawaida huku idadi ya wanafunzi ikiwa ni 1,384 wavulana wakiwa ni 709 na wasichana wakiwa ni 675

Amesema shule hiyo inawafadhili kutoka nchi ya  Finland walioshirikiana na Halmashauri ya Jiji la Arusha lililotoa Sh, milioni 20 na wafadhili wakichangia zaidi ya sh, milioni 180  huku fedha hiyo ikisaidia kujenga jengo bora la ICT na kununua vifaa kama kompyuta mpakato (laptop) 184,deskitopu 5,Projekta 6,Sola 14,Scana Kamera 4,Ipad 22, Mashine ya Laminationi na printa 4.

Pia vijana viziwi wanne wamepata ajira katika kitengo hicho hukuwakimshukuru Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia kwa kuwawezesha kupata maendeleo hayo shuleni hapo

Gambo alimpongeza walimu na wanafunzi wa shule hiyo kwa kutoa elimu kwa wanafunzi wenye ulemavu na kuwasihi walimu kuongeza juhudi za kutoa elimu kwa wanafunzi hao ili waweze kupata ajira na kujikwamua kiuchumi 

Awali Rc Gambo alijionea jinsi wanafunzi hao viziwi wakiimba wimbo wa Taifa kwa kutumia alama zao wakiongozwa na walimu wao ambao ni Veola Wilson na Neema Lema 

Gambo anaendelea na ziara yake ya siku tano Jiji hapa kwa kuzindua miradi mbalimbali ikiwemo uzinduzi wa barabara ya Mahakama na St, James uliogharimu Sh milioni 586. pamoja na kuzungumza na wananchi ili kutatua kero zao

Gambo amewaagiza watumishi wa jiji la Arusha wakiwemo wataalam wa vitengo mbalimbali kuhakikisha wanatatua kero za wananchi haraka iwezekanavyo ili kuondokana na kero zinazowakabili.

 Miradi iliyokaguliwa ni pamoja   na  Visima viwili  vya maji vilivyoko magereza vilivyogharimu milioni 372, madarasa 6 Shule ya msingi Olasity,madarasa 4 ya Shule ya msingi Burka Estate ambayo yamegaharimu jumla ya  shilingi 218 milioni .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad