HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 13 April 2017

Rais Magufuli Ampigia Simu Mwana FA na Kumpongeza

Msanii wa Hip hop Tanzania Hamis Mwinjuma maarufu kama mwana FA jana alielezea alivyofurahishwa na simu aliyoipokea kutoka kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John pombe Magufuli akizisifia kazi zake.
 
Mwana FA katika ukurasa wake wa twitter aliandika kuwa “Nimefurahi kupokea simu ya Mheshimiwa Rais Magufuli kunisalimia na kuniambia kuwa yeye ni mpenzi wa kazi zangu”
katika kuthibitisha furaha yake, Mwana FA aliandika ujumbe mwingine ambao ni mstari ulioko katika wimbo wake wa iliobamba wa ‘Dume Suruali’ unaosema ‘utoe hela kwani ina TV ndani’ kwa lafudhi ya kisukuma huku akitilia mkazo kwa kuweka herufi kubwa katika neno ‘heRA’ ikiwa ni namna ya kuigiliza anavyoongea Mheshimiwa Rais.
Siyo mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kupiga simu kwa wasanii na kuwapongeza kwa kazi zao. Amekuwa na kawaida ya kupongeza pia vituo vya redio na televisheni na kutoa michango mbalimbali katika kuhamasisha ukuaji wa sanaa nchini.
 
Amewahi kupiga simu Clouds tv kupitia kipindi chao cha ‘Clouds 360’ kinachorushwa kila siku asubuhi na kile cha ‘SHILAWADU’ kinachorushwa siku ya Ijumaa kuanzia saa 3 usiku akiwapongeza watangazaji kwa juhudi wanazozifanya na kuwapongeza.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad