HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, April 15, 2017

NMB washiriki kampeni kuhamasisha vijana uelewa masuala ya fedha

Meneja Mwandamizi Kitengo cha Amana, Bima na Huduma za ziada wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Adili (kushoto) akitoa maelezo namna benki hiyo inavyowakumbuka vijana katika bidhaa zao mbalimbali kwa wageni waalikwa, Mkurungenzi Mkuu wa UN CDF Tanzania, Peter Malika (wa kwanza kulia) na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) walipotembelea banda hilo kwenye uzinduzi wa mjadala kujadili changamoto mbalimbali na kuhamasisha vijana nchini kupata uelewa wa masuala ya fedha. Mkurungenzi Mkuu wa UN CDF Tanzania, Peter Malika (kushoto) akimkabidhi Meneja Mwandamizi Kitengo cha Amana, Bima na Huduma za ziada wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Adili (kulia) cheti kilichotolewa na UN-CDF Tanzania, kwa NMB kwenye kampeni kuwahamasisha vijana kupata uelewa wa masuala ya fedha wakiwa ndani ya banda la Benki ya NMB kujua huduma anuai zinazotolewa na benki hiyo na kuwagusa vijana. NMB imeshiriki kufanikisha kampeni hizo. Baadhi ya wageni waalikwa katika kongamano la kampeni zilizowakutanisha vijana kujadili changamoto mbalimbali, wakipokea vipeperushi ndani ya banda la NMB kwenye kongamano hilo. Baadhi ya wageni waalikwa na vijana wakiwa katika kongamano la kampeni zilizowakutanisha vijana kujadili changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha kupata uelewa wa masuala ya fedha. Meneja Mwandamizi Kitengo cha Amana, Bima na Huduma za ziada wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Adili (kulia) akifurahia cheti kilichotolewa na Mkurungenzi Mkuu wa UN CDF Tanzania, Peter Malika (kushoto) kwenye kampeni kuwahamasisha vijana kupata uelewa wa masuala ya fedha wakiwa ndani ya banda la Benki ya NMB kujua huduma anuai zinazotolewa na benki hiyo na kuwagusa vijana. Nikki Wa Pili (kushoto) akizungumza na vijana walioshiriki kampeni zilizowakutanisha vijana kujadili changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha kupata uelewa wa masuala ya fedha pamoja na kuwaunganisha na taasisi zinazowainua vijana kimitaji. Ofisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Maendeleo ya Vijana, Eliakimu Mtawa (kushoto) akizungumza na vijana walioshiriki kampeni zilizowakutanisha vijana kujadili changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha kupata uelewa wa masuala ya fedha pamoja na kuwaunganisha na taasisi zinazowainua vijana kimitaji. Meneja Mwandamizi Kitengo cha Amana, Bima na Huduma za ziada wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Adili (kulia) akizungumza na vijana katika kampeni zilizowakutanisha vijana na kujadili changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuhamasisha vijana nchini kupata uelewa wa masuala ya fedha pamoja na kuwaunganisha na taasisi zinazowainua vijana kimitaji.

 Na Mwandishi Wetu 

BENKI ya NMB imeshiriki kampeni zilizoendeshwa na Shirika la Kimataifa la Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo UN- CDF zinazowakutanisha vijana pamoja na mashirika mbalimbali yanayofanya kazi kuwahusisha maendeleo ya vijana. Kampeni hizo 'BankTheYouth' zilizowakutanisha vijana na kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili zimelenga kuhamasisha vijana nchini kupata uelewa wa masuala ya fedha pamoja na kuwaunganisha na taasisi zinazowainua vijana kimitaji ili wafikie malengo yao. 

Akizungumza na vijana walioshiriki kampeni hizo, Meneja Mwandamizi Kitengo cha Amana, Bima na Huduma za ziada wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Adili alisema vijana wanapaswa kuungana katika vikundi na kuandaa maandiko ya biashara ambayo yataivutia benki kutoa mikopo ili kuendesha biashara zao. 

Alisema benki ya NMB imekuwa mstari wa bele kuibua bidhaa mbalimbali za kibenki zinazolenga kuwainua vijana hasa elimu ya uelewa masuala ya fedha na namna ya kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba. Aliwashauri vijana kutembelea matawi mbalimbali ya NMB na kujenga urafiki kwa kufungua akaunti na kujiwekea akiba kabla ya kuanza kunufaika na bidhaa mbalimbali zilizoanzishwa kuwasaidia vijana kimitaji. 

"...Ili benki ikuamini lazima ujenge mahusiano mazuri, ujenge urafiki na hii ni pamoja na kuwa na akaunti na sisi. Hatuwezi kukuamini kama hata hauna akaunti na sisi, anza kwa kujenga mahusiano mazuri kwanza nasi ndipo tukuamini...hatuwezi kukukopesha kama haupo karibu na sisi," alisema Adili. 

Kwa upande wake Mkurungenzi Mkuu wa UN CDF Tanzania, Peter Malika aliwataka vijana kushiriki vema katika kampeni hizo pamoja na kukubali kubadilika kulingana na mazingira ya sasa na kutumia fursa zilizopo ili ziwaletee maendeleo. Aliwataka kujadiliana na kuibua changamoto anuai ambazo zimekuwa vikwazo katika maendeleo yao. 

Alisema lazima wajiweke katika vikundi na kufuata utaratibu mzuri utakaowekwa na taasisi zinazosaidia vijana kuelekea katika maendeleo. Aidha aliongeza kuwa vikundi vya vijana lazima vijulikane na kufuata utaratibu rasmi uliowekwa ili viweze kuaminika kwa taasisi mbalimbali zikiwemo za kifedha. Aliwaomba wajiwekee utaratibu wa kujiwekea akiba ili waweze kuaminika zaidi. 

Naye Ofisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Maendeleo ya Vijana, Eliakimu Mtawa aliwataka vijana kujenga uaminifu wa kurejesha mikopo pale wanapopata fursa ya kukopeshwa kwani takwimu zinaonesha fedha nyingi zinazotolewa na Serikali kuwakopesha vijana wapate mitaji wamekuwa hawarejeshi jambo ambalo linatishia uhai wa mifuko hiyo kuendelea kusaidia vijana wengine.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad