HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 3 April 2017

NMB - MAGOMENI KUWAPATIA FURSA MBALIMBALI WAJASIRIAMALI ENEO LA MWENGE JIJINI DAR

Meneja wa Benki ya NMB tawi la Magomeni, Janeth Shango (aliyesimama kushoto) akizungumza na baadhi ya wajasiriamali wanaojishughulisha na kazi za ususi wa mitindo ya nywele katika eneo la Mwenge, Jijini Dar es Salaam kwenye warsha ya siku moja iliyohusu fursa mbalimbali wanazoweza kupata wajasiriamali hao kupitia Benki ya NMB. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki. Warsha hiyo, iliandaliwa na Balozi wa Mpango wa Kuwainua Wanawake Kiuchumi Duniani (Empower Women) kutokea hapa nchini, Doris Mollel.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Victoria inayojihusisha na ujasiliamali wa ubunifu wa bidhaa mbalimbali za mikono, Doresta Mpinzile akionyesha moja ya bidhaa alizobuni kwa baadhi ya wajasiriamali wanaojishughulisha na kazi za ususi wa mitindo ya nywele katika eneo la Mwenge, Jijini Dar es Salaam katika warsha ya siku moja iliyohusu fursa mbalimbali wanazoweza kupata wajasiriamali hao kupitia Benki ya NMB.Wengine pichani ni Meneja wa Benki ya NMB tawi la Magomeni, Janeth Shango, Balozi wa Mpango wa Kuwainua Wanawake Kiuchumi Duniani (Empower Women) kutokea hapa nchini, Doris Mollel pamoja na Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Taasisi ya DMF, Rahma Amood.
Sehemu ya Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Magomeni wakichukua maelezo ya baadhi ya Wajasiriamali wanaojishughulisha na kazi za ususi wa mitindo ya nywele katika eneo la Mwenge, Jijini Dar es Salaam, waliokuwa wakijiunga na Benki hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad