HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 17, 2017

‘Nguvu ya Buku’ yampatia Sh Milioni 10 Christopher Mgaya


Msanii nyota wa filamu Tanzania, Kajala Masanja, kulia akishiriki katika droo ya kwanza ya bahati nasibu ya Ijue Nguvu ya Buku inayoendeshwa na Kampuni ya Biko ambapo ilimpata mshindi wake wa kwanza wa Sh Milioni 10 ambaye ni Christopher Mgaya, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Juhudi Ngolo.
 
‘Nguvu ya Buku’ yampatia Sh Milioni 10 Christopher Mgaya

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

DROO ya kwanza ya kuwania Sh Milioni 10 iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki imempatia donge nono mkazi wa Temeke, Christopher Mgaya na kuweka historia ya kuwa mtu wa kwanza kujinyakulia kitita hicho kutoka kwa mchezo wa bahati nasibu wa Biko.
 
Droo hiyo ilichezeshwa na msanii nyota wa filamu nchini Tanzania, Kajala Masanja akishirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Juhudi Ngolo.
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Juhudi Ngolo kushoto akichezesha droo kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10, ambapo mkazi wa Temeke, Christopher Mgaya aliibuka na kitita hicho. Kulia ni msanii wa filamu, Kajala Masanja, akishuhudia.
 
Akizungumza katika droo hiyo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba jumla ya washindi 2000 walipatikana katika zawadi mbalimbali, huku Mgaya yeye akiibuka kinara wa Sh Milioni 10.

Heaven alisema kwamba baada ya kupatikana kwa mteja huyo, taratibu za kumkabidhi hundi yake ya Sh Milioni 10 unaweka ili mteja huyo apate fedha zake haraka iwezekanavyo.

“Tumeanza vizuri kwa kufanikiwa kumpata mshindi wetu wa kwanza wa Sh Milioni 10 ambapo alicheza bahati nasibu yetu, huku yeye akifanikiwa kuibuka mshindi.
Droo hiyo ya kutafuta mshindi wa Sh Milioni 10 inaendelea
Droo inaendelea kutafuta mtu wa kunyakua Sh Milioni 10

Msanii Kajala Masanja akimpigia simu mshindi wa Sh Milioni 10, Christopher Mgaya jana jijini Dar es Salaam.

“Utaratibu ni ule ule kwasababu kila mtu anaweza kushinda kwa kuinguza muamala kwa Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo ataingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 kwenye kipengele cha lipa bili, huku pia akiingiza namba ya 2456 kama namba ya kumbukumbu ambapo Sh 1000 atakayocheza itampatia tiketi mbili za kushinda hapo hapo au tiketi ya kumuingiza kwenye droo ya kuwania Sh Milioni 10”, Alisema Heaven.

Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Juhudi Ngolo alisema kwamba wameikagua kampuni ya Biko na kuvutiwa na utaratbu wa mchezo wao, hali inayoonyesha kwamba Watanzania wapo salama katika kucheza mchezo huo.

“Nimekuwa mwakilishi wa kwanza kutoka Bodi kusimamia wakati wa kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10 ambapo naamini Watanzania wataamua kucheza zaidi,” Alisema Ngolo.

Naye Mgaya mshindi wa bahati nasibu hiyo ya Sh Milioni 10 alisema haamini kwamba ameshinda Sh Milioni 10 hadi hapo atakapokabidhiwa kitita chake ingawa kimemfanya avuje jasho wakati anatangazwa yeye ndio mshindi.

“Nimefurahishwa kushinda kwangu mshiko wa Biko wa Sh Milioni 10 ambapo siamini kama nimeshinda zawadi hiyo kubwa kutoka kwenye Kampuni ya biko,” Alisema Mgaya.

Kwa mujibu wa Biko, mbali na ushindi wa Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni Moja zinazolipwa kila siku na papo kwa hapo kwenye simu za wateja, ushindi wa Sh Milioni 10 utapatikana kila mwisho wa wiki kwa kuchezesha droo inayokutanisha washiriki wote wa siku za wiki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad