HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 8 April 2017

MTANANGE KATI YA YANGA NA MC ALGER KATIKA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR

Na Zainab Nyamka  Globu ya Jamii

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya kimataifa ya hatua ya mtoano ya kombe la Shirikisho Yanga wamefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya MC Alger ya Algeria.

Mchezo huo uliopigwa leo majira ya saa 10 Alasiri katika dimba la Uwanja wa Taifa ukichezeshwa na mwamuzi kutoka Burundi Louis Hazikumana.

Kipindi cha kwanza kilianza kwa Kila upande kusaka goli la kuongoza lakini umakini wa safu ya ushambuliaji ya Yanga iliyokuwa ikiongozwa na Mzambia Obrey Chirwa ilishindwa kutumia nafasi walizozipata.

Mpaka mapumziko timu zinaingia vyumbani, matokeo yalikuwa ni 0-0. Kipindi cha pili kilianza kwa MC Alger kulisakama lango la Yanga lakini umakini wa safu ya ulinzi ilikuwa makini na kuondosha hatari langoni mwao.

Kocha George Lwandamina anafanya mabadiliko ya kwanza na kumtoa Deus Kaseke ambapo mabadiliko hayo yanaleta tija na katoka dakika ya 61 Thaban Kamosoku anaipatia Yanga goli la kwanza.

Yanga walianza kubadilika na kuendelea kulisakama goli la MC Alger lakini Chirwa anakosa umakini na kukosa magoli ya wazi.

Baada ya matokeo hayo, mechi ya marudiano inatarajiwa kuwa April 15 nchini Algeria ambaoo Yanga inatakiwa kuhakikisha wanatoka na ushindi au sare ya aina yoyote ili kufuzu kuingia hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Obrey Chirwa akiongoka na mpira mbele ya Mabeki wa Timu ya MC Alger ya nchini Algeria, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, unaochezwa hivi sasa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Yanga inaongoza kwa bao 1-0 lililowekwa kimyani na Thaban Kamusoko.
 Wachezaji wa Timu ya MC Alger ya nchini Algeria wakimdhibiti Mshambuliaji wa pembeni wa Timu Yanga, Hassan Kessy, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, unaochezwa hivi sasa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
 Mchezaji wa Yanga, Thaban Kamusoko akijirabu kuchukua mpira mguuni mwa Beki wa Timu ya MC Alger ya nchini Algeria, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, unaochezwa hivi sasa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad