HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 21 April 2017

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt .Kebwe aipongeza TCAA kwa mchakato wa ununuzi wa Rada nne.


 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe S. Kebwe akifungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA ), uliofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa la Magadu, mjini Morogoro.
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe S.Kebwe katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa TCAA baada ya  kufungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA ), uliofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa la Magadu, mjini Morogoro. 
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe S.Kebwe akibadilishana mawazo na Menejimenti ya TCAA baada ya ufunguzi mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA ), uliofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa la Magadu, mjini Morogoro
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe S.Kebwe akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw.Hamza S.Johari baada ya kufungua  mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA ), uliofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa la Magadu, jijini Morogoro.

Na Ally Changwila
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt, Kebwe Stephen Kebwe ameipongeza Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwa  kufanikisha mchakato wa ununuzi wa Rada nne za kuongozea ndege nchini, kutokana na Mamlaka kubana matumizi yake na hivyo kupata fedha za kununulia mitambo hiyo.
Akizungumza wakati wa kufungua Baraza la wafanyakazi la TCAA lililofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa  la Magadu jijini,Morogoro, Dkt Kebwe aliongeza kuwa Rada hizo nne zitaifanya Tanzania kuwa katika nafasi nzuri ya ushindani katika sekta ya usafiri wa anga kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.
“Mafanikio yenu katika kuyafikia malengo yatategemea kila mmoja wenu kutimiza wajibu wake kwa kadri ya uwezo wake”. Aliongeza.
Vile vile Dkt. Kebwe ameipongeza TCAA kwa mafanikio iliyoyapata kwa kufaulu ukaguzi wa Shirika la kimataifa la Usafiri wa Anga-ICAO kwa kufikia asilimia 61.
Dkt Kebwe ameongeza kuwa mafanikio ya TCAA ni mafanikio ya sekta nyingine kwani sekta ya usafiri wa Anga ni kiungo muhimu cha kuziwezesha sekta nyingine za uchumi kama utalii, kilimo na madini na kadhalika kuendelea kukua.
Dkt Kebwe pia ameongeza, Usafiri wa Anga si usafiri wa anasa bali ni usafiri wa msingi kwa kuchochea maendeleo, na kwamba Tanzania inapaswa kufanya jitihada za kuongeza  watoa huduma za usafiri wa anga ikiwa ni pamoja na mashirika ya ndege mengi  kutoa fursa kwa wananchi wengi  kuutumia usafiri huo  kwa gharama nafuu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad