Afisa Usalama katika mgodi wa Dhahabu wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya ACACIA,Samweli Nansika (aliyenyoosha kidole) akitoa maelezo kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda la mgodi huo.
Mkuu wa Idara ya Usalama na uokoaji katika Mgodi wa Dhahabu wa North Mara ,Emanuel Erasto(katikati) akitoa maelezo namna amavyo wanaweza kumuokoa mtu aliyepata athari iliytokana na kemikali.

Maonesho ya Wiki ya Usalama na Afya mahala pa kazi yanayofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro.
Maonesho
haya yanayohusisha kampuni na Taasisi mbalimbali nchini yanaratibiwa na
Wakala wa Usalama na Afya mahala pa Kazi (OSHA).

Baadhi
ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu unaomilikiwa na
Kampuni ya ACACIA,wakiweka sawa moja ya picha inayoonesha eneo ambalo
shughuli za uchimbaji unafanyika.
Afisa
Uhakiki na Usalama katika Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu unaomilikiwa
na kampuni ya ACACIA,Amina Mohamed akitoa maelezo kwa wananchi
waliotembelea banda hilo.
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu unaomilikiwa na
Kampuni ya ACACIA,wakitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda hilo
katika maeonesho ya wiki ya usalama mahala pa kazi ndani ya viwanja vya
Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
Afisa
Afya katika Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu ,Tumaini Sylivanus akitoa
maelezo ya namna wanavyotoa huduma ya Afya kwa wafanyakazi wa Mgodi huo
pindi wapatapo matatizo.
Mmoja
wa Wakazi wa Kilimanjaro akipewa maelekezo ya namna ya kutumia kifaa
maalumu kinachotumika katika zoezi la uzimaji wa moto pindi yatokeapo
majanga ya Moto.Nyuma yake ni mmoja wa wafanyakazi wa Mgodi wa
Bulyanhulu unaomilikiwa na kampuni ya ACACIA.
Afisa
Viwango wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu,Setieli Kimaro akitoa
ufafanuzi kwa wananchi waliotembelea banda la modi huo unaomilikiwa na
kampuni ya ACACIA.
Afisa
Usalama katika Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya
ACACIA,Deogratius Nyantabano akitoa maelezo kwa wanafunzi waliotembelea
banda la mgodi huo katika maonesho ya wiki ya usalama na afya mahala pa
kazi yanyofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi
,Kilimanjaro.
Afisa
Usalama katika Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya
ACACIA,Mustapher Mlewa akieleza jambo kwa baadhi ya wananchi
waliotembelea Banda hilo.
Daktari
kutoka Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,Dkt Ludovick
Silima akitoa maelezo juu ya usalama kwa mmoja wa wananchi waliofika
katika banda la mgodi huo wakati wa maonesho ya wiki ya usalama na afya
mahala pa kazi yanayoendelea katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika
Moshi.
Afisa
Mazingira katika Mgodi wa north Mara ,Sara Cyprian akionesha picha na
maelezo kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda la Mgodi huo katika
maonesho ya wiki ya usalama na afya mahala pa kazi.
Eneo maalumu la kumuogesha mtu aliyepata athari ya kemikali.
Afisa usalama akita huduma ya kumsafisha mtu aliyepata athali ya kemikali akiwa nje ya bafu hilo la kumuogeshea ili na yeye asipate madhara.
Wafanyakazi wa Mgodi wa Buzwagi wakionesha namna ambavyo wanaweza msaidia mtu aliyepatwa na janga la Moto.
Kifaa Maalumu kinachotumika katika kubeba mwili wa mtu aliyepata madhara akiwa katika shimo wakati wa uchimbaji wa Dhahabu.
Mmoja wa wafanyakazi wa Mgodi wa Bulyanhulu akitoa maelezo kwa wananchi walitembelea banda hilo namna ambavyo wanaweza kunyanyua Gari pamoja na Mawe yaliyomuangukia mtu wakati akitekeleza majukumu yake kwa kutumia kifaa maalumu kinachojazwa upepo (Air Bag).
Mkuu wa Idara ya Usalama na Uokoaji katika Mgodi wa North Mara ,Emanuel Erasto akitoa maelezo namna wanavyoweza kumukoa mtu aliyepatwa madhara akiwa chini ya mgodi .
Dkt Ludovick Silima akitoa ufafanuzi kwa wananchi waliotembelea banda la Mgodi wa Buzwagi.
Afisa Mahusiano katika Mgodi wa Bulyanhulu akitoa maelezo ya namna Mgodi huo unavyo tekeleza majukumu yake ukitoa kipaumbele katika masuala ya Usalama na Afya kwa watumishi wake.
Afisa Uhusiano wa Mgodi wa Buzwagi ,Magesa Magesa akitoa maelezo namna mgodi huo ulivyoshiriki katika shughuli za maendeleo ikiwemo ujengaji wa vyumba vya madarasa,zahanati,maji pamoja na suala la kuhamasisha michezo katika maeneo yanayozunguka mgodi huo.
Na Dixon Buagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
No comments:
Post a Comment