HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 5 April 2017

MANISPAA YA UBUNGO YAFANYA OPERESHENI MAALUM YA UKUSANYAJI MAPATO MANZESE.

Manzese, Dar es Salaam.
Kamati ya fedha na uongozi kwa kushirikiana na wakuu wa  idara na timu ya ukusanyaji mapato halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wamefanya operesheni maalum ya kukagua leseni za biashara, leseni za vileo, kodi ya huduma ya jiji (city service levy), ushuru wa nyumba za kulala wageni ( hotel levy), ushuru wa  mabango, vibali vya ujenzi, TFDA,  ukusanyaji wa mapato na kuelimisha wafanyabiashara juu ya umuhimu wa kulipa kodi katika mitaa mbalimbali ya Kata ya Manzese.

Kamati hiyo inayoongozwa na mwenyekiti Mstahiki Meya Boniface Jacob na katibu ambaye ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndg. John Lipesi Kayombo kwa kushirikiana na watumishi hao imefanya  operesheni hiyo leo kwa lengo la kuhamasisha ulipaji wa  kodi, ada na tozo mbalimbali za Manispaa ya Ubungo.

Wakati wa  operesheni hiyo changamoto mbalimbali zimejitokeza zikiwemo wafanyabiashara kutokuwa na uelewa juu ya ukataji wa leseni, kutokukata leseni kwa wakati na kutokuweka leseni katika eneo la biashara.

Akizungumza wakati wa operesheni hiyo mwenyekiti wa kamati Mstahiki Meya Boniface Jacob aliwasisitiza wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati na hatimaye kuleta maendeleo katika Manispaa ya Ubungo na taifa kwa ujumla.

"Ndugu wafanyabiashara kulipa kodi ni wajibu wenu kwani itawasaidia ninyi wenyewe na vizazi vyenu na  unapolipa kodi ndipo tutaweza kujenga zahanati, shule, masoko na huduma muhimu katika Manispaa yetu" alisema Meya Boniface Jacob.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad