HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 13, 2017

IDADI YA WABUNGE WALIOPEWA VITISHO NA WATU WASIOJULIKANA YAZIDI KUONGEZEKA.

Idadi ya wabunge waliopewa vitisho na watu wasiojulikana imezidi kuwa hadharani baada ya majina ya wabunge wengine wanne wapya kutajwa bungeni kuwa ni miongoni mwa wabunge ambao maisha yao yapo hatarini na hivyo wanaliomba bunge kushughulikia usalama wao kwani hawajui kwa sasa watafanyaje ili kujinusuru kutoka katika hatari hiyo.

Wakiomba miongozo ya kiti Mhe. Mwita Waitara mbunge wa Ukonga alitaja majina ya wabunge wanne ambao alitumiwa majina kupitia ujumbe wa mfupi wa simu kuwa wanasakwa huku Mhe. Dkt. Godwin Molley mbunge wa Siha naye aliomba muongozo wa kiti kutaka bunge liahirishwe ili wajadili hali hiyo hata hivyo kiti kilikataa miongozo hiyo.

Mhe. Said Kubebea ni mbunge kutoka Ubungo ambaye anasema kilio cha wabunge kuhusu kuhakishiwa usalama wao ni jambo ambalo mtu yoyote hapaswi kukipuuza kauli ambayo inaongezewa nguvu na Mhe. Mwigulu Nchemba waziri wa mambo ya ndani ya nchi anasisitiza usalama upo huku waziri wa habari utamaduni sana na michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akimjibu Mhe. Juma Mkamia kuhusu yeye kushiriki mkutano wa mwanamuziki Roma Mkatoliki.

Katika hatua nyingine wabunge wamepata nafasi ya kuchangia hotuba ya waziri mkuu ikiwa ni katika hatua za kuhitimisha ambapo wabunge wengi wamesema kama bajeti itatekelezwa kama ilivyopangwa itakuwa msaada mkubwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad