HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 24 April 2017

DC NJOMBE,RUTH MSAFIRI AONYA MABARAZA YA KATA KUTENDA HAKI, AWEKA JIWE LA MSINGI OFISI YA KATA YA KITISI-MAKAMBAKO..


Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Ruth Blasio Msafiri akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mdogo Makambako na Diwani wa Kata ya Kitisi (CCM) Mjini Makambako Mhe. Navy Sanga wakikagua Jengo la Ofisi ya Serikali ya Kata hiyo


Ripoti fupi kuhusu Ujenzi wa Ofisi za Serikali Kata ya Kitisi iliyogharimu jumla ya Shilingi za kitanzania Milioni 16 ilisomwa na Afisa Mtendaji Kata ya Kitisi Ndugu Albert Minja imeonyesha zaidi ya Shilingi milioni 11 ni fedha za wananchi walizochanga huku kiasi baki kikiwa kimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Makambako Mhe. Deo Sanga "Jah People",  Wadau mbalimbali wa maendeleo na Fedha kutoka mfuko wa Jimbo. 
Katika hotuba yake DC Ruth Msafiri amezungumzia ni kwa jinsi gani Serikali ya Kata ya Kitisi itaweza kuendesha shughuli zake kwa uhuru zaidi huku akiwaonya wajumbe wa Mabaraza ya Kata kuepukana na upendeleo kwenye maamuzi, rushwa na ubadhilifu wowote kwani Mabaraza hayo kwa maeneo mengine ndiyo yamekuwa yakikwamisha shughuli za maendeleo. 
Aidha, Mkuu wa Wilaya hiyo alitumia sehemu ya maongezi yake kuwaasa wananchi kufanya kazi kwa bidii huku akiwapa nguvu pia wanawake kuhakikisha hawabweteki. Licha ya kuzungumza hayo pia DC Msafiri amewakumbusha Viongozi na wananchi kwa ujumla wao kujitokeza kwenye Sherehe za Upokeaji wa Mwenge zitakazofanyika siku za hivi karibuni Wilayani hapo. 
Diwani wa Kata ya Kitisi Mhe. Navy Sanga (kulia), akimuonesha namna Ujenzi ulivyo kamilika Mkuu wa Wilaya Mhe. Ruth Msafiri 
DC Msafiri akitoa maelekezo kwa Viongozi wa Kata ya Kitisi wakati akihitimisha shughuli ya kukagua Jengo hilo
 Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Ruth Msafiri akijumuika kucheza kwaya na Kikundi cha akina Mama cha Bwawani Beach wakati akiwasili Katani Kitisi, Mjini Mdogo wa Makambako
HATIMAYE IMEKUWA: DC Msafiri akifurahi mara baada ya kukata utepe kama Ishara ya kuweka rasmi Jiwe la Msingi kwenye Ofisi ya Serikali ya Kata ya Kitisi
Afisa Mtendaji wa Kata ya Kitisi Ndugu Albert Minja akisoma Ripoti ya Ujenzi wa Ofisi hiyo iliyoanza kujengwa Mwezi Disemba, 2016
Akina Mama wa Kikundi cha Bwawani Beach wakishirikiana na Diwani wa Kata ya Kitisi Mhe. Navy Sanga wakimzawadia Mkuu wao wa Wilaya Zawadi ya Kitenge
Wananchi wa Kata ya Kitisi wakimsikiliza Mkuu wao wa Wilaya na Diwani wao
Afisa Tarafa ya Makambako Mhe. Barthromew Mwella Mwellange akizungumza wakati wa Uwekaji Jiwe la Msingi Ofisi ya Kata ya Kitisi

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad