HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 14 April 2017

Dasani Marathon 2017 kufanyika mei 14 jijini Dar

                          Dar Running Club ikishirikiana na Kampuni ya maji ya kunywa Dasani, leo imeanza kufanya usajili kwa washiriki  wa mbio za km 10 na 21km zijulikanazo kama Dasani Marathoni zitakazofanyika Jumapili  ya Mei 14, 2017 jijini Dar es Salaam.
Hii ni mara ya tatu sasa kwa Dar Running Club kuendelea kuihamasisha jamii kufanya mazoezi kwa kuandaa mashindano haya, ambayo yatafanyika tarehe  Jumapili  ya Aprili  2017. Awali mashindano haya yalikuwa yakijulikana kama May Day Marathon lakini kutokana na kushirikiana na kampuni ya maji ya Dasani kuyaandaa mwaka huu yatajulikana kama Dasani Marathon 2017.
Akizungumzia mashindano haya, Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Coca-Cola Kwanza LTD, kampuni ya inayotengeneza maji ya Dasani, Nalaka Hettiarachchi amesema kuwa maji ya kunywa ya Dasani ni murua na yenye kuondoa kiu, hususani wakati wa kufanya mazoezi au unapojisikia kuburudika na ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kushiriki kwa wingi ili kujenga afya zao kwa mazoezi. 
 Pia akiamini kuwa tunaweza kuleta uzoefu mkubwa kwa wahsiriki na kulifanya kuwa tamasha la kukumbukwa. Pia tutalifanya tukio hili kuwa maarufu zaidi na lakusisimua kwa miaka ijayo likiwa na vivutio vingi kwa washiriki kutoka katika matembezi mbali mbali”. Lengo letu kubwa ni kusaidia vijana na kuhamasisha Watanzania wenye vipaji kufikia viwango vya Kimataifa and kuleta heshima kwa nchi yako… aliongeza Nalaka
Kwa upande wake, rais  wa Dar Running Club,  Goodluck Elvis, alisema kauli mbiu ya klabu yao ni "Active. Wherever. Whenever" na  imefarijika kuungana na Dasani katika kuandaa mashindano haya Dasani Marathon 2017 ambayo umaarufu wake umekuwa ukiongezeka kwa kasi mwaka hadi mwaka.
Kama ilivyokuwa kwenye mashindano ya miaka miwili iliyopita, mbio hizo zitaanzia na kumalizikia  Police Officers Mess Oysterbay. Mbio za 21km zitaanza saa kumi na mbili kamili alfajiri, zikifuatiwa na zile za 10km ambazo zitaanza saa kumi na mbili na nusu asubuhi. Washindi watano wa mbio za 21km na washindi watatu wa mbio za 10km watazawadiwa zawadi nono ikiwemo fedha taslimu.
Kiwango cha kusajili ni TZS 30,000/= kwa mbio zote na mwisho wa usajili ni tarehe 13 Mei, 2017.
Vituo vya awali vya usajili vitakuwa  Colosseum Gym - Masaki, Shoppers plaza – Mikocheni, China Plaza: Ghorofa ya 11 mtaa wa Uhuru na Mheza Kariakoo na Mlimani City Mall. Washiriki wote watafanikiwa kupata fulana zenye kiwango cha juu na vilevile watazawadiwa medali pindi watakapokamilisha mbio hizo kwa wakimbiaji elfu moja wa kwanza.

Kwa Taarifa Zaidi wasiliana na:
Goodluck Elvis, Dar Running Club  President, 0715 302 336
Erick Kahwa, Dar Running Club  Secretary, 0784024422


Dorothy Kipeja, Dasani Marathon Marketing Manager  0754 291 291

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad