HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 1 April 2017

BOKO BEACH VETERANS YAISAMBARATISHA GYMKANA VETERANS KWA BAO 3-1

 Timu ya Boko Beach Veterans (BBV) imefanikiwa kuwasambaratisha Veterans wa Gymkana kwa ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa jana jioni katika viwanja vya Gymkana, jijini Dar es salaam.

Wakicheza kwa kujiamini na uelewano mkubwa Maveterani kutoka Boko walionekana kuutawala sana mchezo huo na kuwapa tabu wapinzani wao Gymkana walioonekana kuicheza mechi hiyo kwa hofu. 

Boko waliianza karamu hiyo ya mabao mnamo Dakika Saba ya mchezo kufuatia krosi maridadi toka kwa nyota wake machachari Malekano (messi wa Boko) kutua kifuani kwa Charles Palapala na kuutupia nyavuni kwa ufundi mkubwa, Goli hilo lilidumu hadi mapumziko. 

Kipindi cha pili kilianza kwa Veterans wa Gymkhana waliokua wakiongozwa na Nahodha Ally Mayai Tembele, Juma Pinto, Mohd Sebene na kiungo asiekabika Makocha Tembele walilishambulia lango la Boko beach Veterans kama nyuki na hatimae wakasawazisha kupitia kwa Mshambuliaji wao Mohd Sebene baada ya beki wa boko Kitwana Mango kucheza rafu nje ya kumi na nane.
Baada ya kusawazisha goli hilo, Timu ya Gymkana Veterans walionekana kuridhika kimchezo na hivyo kuwapa nafasi Boko Beach kutawala kiungo iliyokua ikiongozwa na Kudra Omary, Engenier Kamugisha, Elimboto Nkumbi na Hebron Malakasuka na hatimae kuongeza magoli mawili ya haraka haraka katika dakika ya 65 na 78 kwa magoli mazuri ya kiufundi yaliyowekwa kimiani na Elimboto Nkumbi, huku goli la lingine likifungwa na beki Mohamed Mwinchumu baada ya kazi nzuri iliyoanzishwa na kiungo Kudra Omari.

Huo unakuwa ni ushindi wa pili ndani ya siku saba baada ya mchezo wa kwanza kuirarua Timu ngumu ya veteran ya AZAM magoli matatu kwa mawili.

BBV watakua na kibarua kingine kigumu siku ya jumapili (Aprili 2) katika uwanja wake wa nyumbani watakapo ikaribisha Timu nyingine ngumu ya Dar City FC yenye nyota wa zamani kama George Masatu, Akida Makunda, Clement Kahabuka, Ally Mpemba, Zubeir Zatwila, Salvatory Edwards na Kiungo hatari Ernest Nyambo na Ally Kakima.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad