HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 6 March 2017

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO, NAPE NNAUYE MAENDELEO YA MKURANGA YATAPATIKANA KWA JUHUDI YA WANAMKURANGA WENYEWE

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema michezo inajenga umoja wa kitaifa na kuondoa ubaguzi katika jamii.
Waziri Nape ameyasema hayo  wakati wa Fainali ya Ulega Cup iliyofanyika kwenye kiwanja cha shule msingi Mkuranga,  amesema licha ya micheszo kuhamasisha umoja na furaha kwa jamii pia ametaka ihamasishe na shughuli zingine za maendeleo.
Amesema katika jitihada za Mkuranga kuwa na kiwanja cha mpira ataunga mkono mara baada ya kupata mchoro wa ramani ili na Mkuranga iwe na kiwanja cha kuweza kucheza mechi ya Ligi Kuu.
Amesema maendeleo ya Mkuranga yatapatikana kwa juhudi ya wanamkuranga wenyewe.
Katika fainali hiyo Waziri amechangia shilingi laki 300,000/=  kwa  timu tatu kupata laki moja kwa mshindi wa kwanza wa pili na watatu.
 Fainali hiyo imechezwa  kati ya timu ya Kisiju na Tengera ambazo zilitoka sare ya bila kufungana  ambapo zilikwenda katika hatua ya matuta na kuibuka kwa timu ya Tengera kwa mabao matatu dhidi ya timu ya kisiju iliopata magori mawili.
Waziri Nape amesema mashindano yajayo atamuunga mkono mbunge kupata wadhamini wa katika kuendesha mashindano hayo. Nae Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amesema vijana wameonyesha vipaji ambayo vinatakiwa kuendelezwa
 .Waziri wa Habari, Utamaduni , Michezo na Sanaa, Nape Nnauye akizungumza katika fainali za Ulega Cup iliyofanyika katika kiwanja cha mpira cha shule ya msingi Mkuranga.
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga akizungumza katika fainali za Ulega Cup kuhusu juhudi zake katika kuleta maendeleo jimbo kwake na udahmini wake wa kuanzisha mashindano hayo.
Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza kuhusu maendeleo ya jimbo lake na lengo la kuanzisha Kombe la Ulega ambapo fainali za kombe hilo zimefanyika jana kwenye Wilayani ya Mkulanga.
Waziri wa Habari, Utamaduni , Michezo na Sanaa, Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na timu ya Tengera mkoani Pwani.
Waziri wa Habari, Utamaduni , Michezo na Sanaa, Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na timu ya Kisiju mkoani Pwani.
Waziri wa Habari, Utamaduni , Michezo na Sanaa, Nape Nnauye  Picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoani Pwani.
Mechi ikiendeleaa

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad