Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto Mhe Ummy Mwalimu ameagiza
kuanzishwa duka la Dawa ndani ya miezi 3 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Iringa.
Hayo
ameyasema wakati wa ziara ya kikazi
mkoani Iringa leo tarehe ambapo ametembelea Kituo cha Damu Salama cha Mkoa pamoja na Hospitali ya
wilaya ya Mafinga
“Pia
naagiza Uongozi wa Hospitali zote za
Mikoa na Wilaya kuanzisha Wodi za Watoto Wachanga na Watoto Njiti mara moja” alisema
Mh. Ummy.
Mbali
na hayo Waziri Ummy ameagiza kujengwa
kwa Kitengo cha Wagonjwa wa Dharura
(Emergency Unit) kwa hospitali hizo mara moja ili kuboresha huduma ya afya kwa
wakazi wa Iringa.
Akitoa taarifa ya utoaji wa huduma za Afya
katika mkoa mbele ya Waziri wa Afya, mhe. Amina Masenza, mkuu wa Mkoa wa Iringa
alieleza hatua mbalimbali wanazochukua katika kuboresha utoaji wa huduma
ikiwemo kuboresha miundombinu ya vituo vya Afya, upatikanaji wa dawa, vifaa na
vifaa tiba, utoaji wa elimu ya uzazi wa mpango pamoja na lishe kwa wananchi
bila kusahau kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).
Hata
hivyo, zipo changamoto kadhaa zinazowakabili mkoa kufikia lengo la lao kutoa
huduma bora za Afya. Mathalani katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Iringa
haina wodi/kitengo cha dharura, upungufu wa watumishi, Ufinyu wa eneo la
Hospitali, ukosefu wa Gari la Kubebea Wagonjwa na ukosefu wa baadhi ya
vitendanishi.
Mhe.Ummy
Mwalimu amewapongeza viongozi na watumishi wa mkoa kwa juhudi kubwa wanazofanya
katika kuboresha huduma za afya ikiwemo kufanikisha ujenzi wa wodi ya watoto
waliozaliwa kabla ya wakati na watoto wachanga. Wodi hiyo yenye vifaa vyote
muhimu imejengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya ASAS ya Mjini Iringa.
Mhe Ummy
amewataka wadau wengine waendelee kusaidia sekta hii hususani eneo la Afya ya
Mama na Mtoto kwa kuwa linawagusa wananchi wengi hasa wa kipato cha chini.
Kufuatia
malalamiko aliyoyapokea kutoka kwa wananchi waliofika kupata huduma katika
Hospitali ya Rufaa ya mkoa, Mhe.ummy aliagiza utekelezaji wa masuala yafuatayo;
ujenzi wa wodi ya wagonjwa wa dharura na duka la dawa la Hospitali ili kuondoa
usumbufu wanaoupata wagonjwa wa kwenda kununua dawa kwenye maduka binafsi.
Pia,aliahidi kulifuatilia suala linalohusu gereza lililopo jirani na Hospitali
ya mkoa ili liweze kuhamia sehemu nyingine na kutoa eneo kwa Hospitali. Vile
vile, ametoa muda wa miezi 9 kuanzia leo tarehe 16 March kwa wakurugenzi wa
Halmashauri zote Nchini kuhakikisha vituo vyote vya Afya vinatoa huduma kamili
za uzazi za dharura ikiwemo upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni.
Akiwa
katika Hospitali ya wilaya ya Mufindi, mhe. Ummy aliagiza yafuatayo; uongozi wa
wilaya uhakikishe maji yanapatikana muda wote hospitalini, waanzishe mara moja
wodi maalum kwa ajili ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati na Watoto wachanga.
Pia, aliwakumbusha juu kuhakikisha kuwa wazee wote wanatambuliwa na kupewa
vitambulisho lakini alipongeza juhudi zinazofanywa na Halmashauri ya Wilaya ya
kuwakatia Wazee kadi za Bima (TIKA).
No comments:
Post a Comment