HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 19 March 2017

WASHINDI MICHUANO YA GOFU YA BRITAM WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

Zaidi ya wachezaji 100 walishiriki michuano hiyo ya gofu ya Britam huku Adam Ngamilo akiibuka mshindi wa jumla baada ya kupata pointi 39 katika mashimo 18 aliyocheza katika klabu ya Gymkhana Dar es Salaam.

Aidan Nziku alikuwa mshindi kwa upande wa wanaume, akipata pointi 37 na Mary Kinusia akiibuka mshindi kwa upande wa wanawake baada ya kupata pointi 38.

Mkurugenzi Mtendaji wa Britam Tanzania, Steven Lokonyo amesema watadhamini tena michuano hiyo ili kuendeleza gofu na michezo mingine klabuni hapo.
" Kampuni yetu ipo Afrika yote ya Mashariki na huko kote tunadhamini michezo".

" Nchini Kenya tunadhamini michuano ya wazi ya Safari ya Tennis ( Safari Open ) na klabu ya Mathare United, Hii ni sehemu tu ya mchango wetu", alisema bosi huyo wa kampuni hiyo inayojihusisha na aina zote za bima.

Amesema kampuni yake ina wataalamu waliobobea katika masuala ya bima zote na siku zote wateja wao wamekuwa katika mikono salama.
"Popote upo salama ukiwa na Britam, tunatoa aina zote za bima kwawatu binafsi, vyombo vya moto, bima kwa wasafiri, wachezaji, majengo na vingine vingi ikiwa bima ya afya ambayo iko mbioni kuanzishwa", alisema Lokonyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad