HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 12 March 2017

WANANCHI WALIOJENGA NYUMBA KATIKA RELI YA TRL WAVUNJIWA NYUMBA ZAO

 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Nyumba zaidi ya 200 zilizojengwa ndani ya Reli ya TRL kuanzia Ilala , Bunguruni, pamoja na Mnyamani zimevunjwa.
Akizungumza na waandishi habari, Catherine Moshi amesema kuwa kabla ya kuvunja nyumba hizo wananchi walitarifiwa uvunjwaji huo na taratibu za kisheria zilifuatwa.
Catherine amesema wananchi hao walikaa kwa muda mrefu katika maeneo hayo lakini wanavuja kutokana  na ujenzi wa Reli ya Standard Gauge na jiwe la msingi litawekwa hivi karibuni.
Amesema katika kufanya ujenzi wa reli hiyo hawataki usumbufu kwa wakandarasi kupata kikwanzo kutokana na makazi yaliyojengwa katika reli hiyo.
Baadhi ya wananchi wamesema kuwa uvunjaji huo haujafuata taratibu na muda waliombiwa ni mdogo katika kujiandaa kutoa vitu vyao.
Mkazi wa Bunguri aliovunjiwa nyumba, Said Abdallah amesema kuwa wamepata pigo kuvunjwa nyumba hizo na muda uliotolewa ni mdogo.
 Tingatinga likiomoa nyumba zilizojengwa katika reli leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
 Baadhi ya vyombo vikiwa nje baada ya kuvunjwa nyumba zilizo katika reli leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wananchi wakatoa vitu mbalimbali katika nyumba ambazo zimenjengwa katika reli leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wananchi waliokuwa wakishuhudia ubomoaji wa nyumba zilizojengwa  katika reli jijini Dar es Salaam.Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad