HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 4, 2017

WANAFUNZI WAUGUZI WA CHUO KIKUU CHA WRIGHT, JIMBO LA OHIO MAREKANI WATEMBELEA SKULI YA AFYA NA SAYANSI ZA TIBA YA SUZA MBWENI.

Kaimu Mkuu wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Amina Abdulkadir akizungumza na wanafunzi wauguzi wa Chuo Kikuu cha Wright Jimbo la Ohio nchini Marekani walipotembelea Skuli hiyo Mbweni kubadilishana uzoefu.
Mwanafunzi Muuguzi kutoka Chuo Kikuu cha Wright nchini Marekani Melissa Vanscoy akieleza lengo la ziara yao hapa Zanzibar wakati wanafunzi wa vyuo hivyo viwili walipokutana katika Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya SUZA Mbweni.
Wanafunzi wauguzi wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya SUZA wakibadilishana mawazo na wanafunzi wenzao wa Chuo Kikuu cha Wright kutoka Jimbo la Uhio Marekani walipowatembelea skulini kwao Mbweni.
Wanafunzi wauguzi kutoka Chuo Kikuu cha Wright na SUZA wakiwa katika darasa la kufanyia mazoezi ya vitendo wakielekezana namna ya kumuhudumia mgonjwa alielezwa wodini.
Picha ya pamoja ya wanafunzi wauguzi wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya SUZA wakiwa na baadhi ya walimu na wenzao wa Chuo Kikuu cha Wright, Jimbo la Uhio nchini Marekani wakiwa katika kempasi ya Mbweni.

Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad