Timu
ya Vijana U17 ya Burudi leo asubuhi imefanya mazoezi kwenye Uwanja wa
Kaitaba kujiweka kisawasawa na kuusoma uwanja huo ili kujiimarisha vyema
kabla ya kukutana uso kwa uso leo na Timu ya Tanzania ya vijana wenye
umri wa miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys. Timu hii itacheza
michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini
Bukoba mkoani hapa Kagera. Timu hii itacheza michezo miwili ya
kirafiki ya kimataifa
kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani hapa Kagera. Mchezo wa
kwanza utaanza kuchezwa leo hii Machi 30, 2017 na kurudiana Aprili
mosi, mwaka huu. Hata hivyo Mvua iliweza kunyesha na kukatisha zoezi
lao asubuhi na hatimae kurudi kwenye makazi waliyofikia jana baada ya
kuchelewa kufika Bukoba na kutoweza kufanya mazoezi kwenye uwanja huo.
Nayo
Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya vijana wenye umri wa miaka 17
maarufu kwa jina la Serengeti Boys jana Jamatano walifanya mazoezi
asubuhi saa nne kujiweka tayari na mchezo wao wa leo na Timu hii ya
Burundi.
Serengeti
Boys itakuwa kambini mjini hapa Bukoba hadi Aprili 2, mwaka huu ambako
Serengeti Boys ambayo inajiandaa na michuano Afrika huko Gabon itarejea
Dar es Salaam Aprili 2, mwaka huu ambako imepangwa kucheza na Ghana
Aprili 3, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo
utatanguliwa na hafla ya kuagwa kwa kukabidhiwa bendera.
Mvua kubwa ilinyesha na kukatisha Tizi lao kwenye Uwanja huo wa Kaitaba asubuhi hii na kwenda jukwaa kuu
Wakisikilizia Mvua...
No comments:
Post a Comment