HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 2 March 2017

SIMBA WAINGIA MAWINDONI KUSAKA POINTI 3 ZA MBEYA CITY JUMAMOSI


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Kikosi cha Simba kimeeendelea na mazoezi katika viwanja vya Chuo cha Polisi Kilwa Road kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa l.igi kuu dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Jumamosi kwenye dimba la Uwanja wa Taifa.

Simba ambayo ipo kambini toka jana jioni, inajifua zaidi ili kuweza kutoka na ushindi kwenye mchezo huo ambapo wapo katika mbio za kuutafuta ubingwa wa ligi kuu Vodacom msimu wa 2016/2017.

Wanamsimbazi hao ambapo katika mechi yao ya mwisho dhidi ya Yanga waliweza kuvuna alama tatu na kufikisha alama 54 wakiwa wamejikwea kileleni wakifuatiwa na mahasimu wao wenye alama 52 baada ya ushindi walioupata kwenye mchezo wao wa kiporo dhidi ya Ruvu Shooting.

Kocha msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja ameweka wazi kuwa bado hawawezi kusema wameshakuwa mabingwa kwabni ligi ya msimu huu ni ngumu sana na haitabiriki kwani kila timu imejizatiti kutoka na ushindi.

Mayanja amesema kuwa, kwa sasa kila kitu ni kuangalia namna gani wanashinda kwenye michezo iliyobaki ili kujihakikishia wanatoka na ubingwa msimu huu na zaidi kila mchezaji anajua nini wanakitaka ambapo ni ubingwa tu. 

Kwa sasa viongozi wa Simba wanataka kuhakikisha wanachukua ubingwa ligi msimu huu baada ya kukaa miaka minne bila kuchukua kombe na kushindwa kushiriki michuano ya kimataifa.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad