HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 17 March 2017

SEMINA ENDELEVU YA BODI YA USAJILI WA WABUNIFU MAJENGO NA WAKADIRIAJI MAJENZI YA 27 KUFANYIKA MWANZA

 Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Arch, Dk.Ambwene Mwakyusa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana maandalizi ya semina endelevu ya Bodi ya 27, itakayofanyika tarehe 23-24, machi 2017 katika ukumbi wa Rock City Mall Mwanza.

Ambapo amesema lengo la semina hiyo ni kuwaelimisha Wabunifu Majengo, Wakadiriaji Majenzi na Wataalam wanaoshabihiana nao pamoja na wadau kutoka sekta ya ujenzi ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknologia na kubadilishana changamoto za utandawazi.

Mgeni rasmi katika semina hiyo anatarajiwa kuwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.

KAULI MBIO YA SEMINA HIYO.

"Mchango Unaotokana na Ushirikiano wa Serikali na Sekta Binafsi, Pamoja na Taasisi za Fedha katika kuendeleza Sekta ya Ujenzi ('The Contribution of Public Private Partneship anda Financial Institutions in the Development of the Construction Industry)
QS Albert munuo. Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi akiwaelezea waandishi wa habari mada zitakazotolewa katika semina hiyo endelevu ya Bodi ya 27, itakayofanyika tarehe 23-24, machi 2017 katika ukumbi wa Rock City Mall Mwanza (kulia) Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Arch. Dk.Ambwene Mwakyusa. Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Arch. Dk.Ambwene Mwakyusa akijibu maswali kwa waandishi wa habari wa kuhusiana maandalizi ya semina endelevu ya Bodi ya 27, itakayofanyika tarehe 23-24, machi 2017 katika ukumbi wa Rock City Mall Mwanza. Mmoja wa waandishi wahabari (kushoto) akiuliza swali wakati wa mkutano mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad