HABARI MPYA

Home Top Ad



Post Top Ad

Thursday, 9 March 2017

RITA KUBORESHA MFUMO WA USAJILI WA KUTOA VYETI VYA KUZALIWA KWA WATOTO KUPITIA MPANGO WA CRVS

Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) umeandaa maboresho ya ujumla ya mfumo mzima wa usajili chini ya Mkakati wa Kitaifa wa Kuboresha Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu na Takwimu (National Strategy on Civil Registration and Vital Statistics - kwa kifupi National CRVS Strategy), ili kuisaidia Serikali kupata takwimu sahihi za wananchi zinazoisaidia kupanga mipango ya maendeleo na huduma za jamii. Kwa mujibu wa Takwimu za Sensa ya mwaka 2012 ni asilimia 13.4 ya Wananchi ndiyo waliyosajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa.

Hayo yamesemwa na Kaimu Afisa Mtendaji wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Emmy Hudson, wakati wa Mkutano wake na baadhi ya wahariri na waandishi wa habari, uliofanyika kwenye makao makuu ya RITA, jijini Dar es salaam.

Alisema Mkakati huo wa CRVS una mipango mbalimbali ya utekelezaki ikiwa ya muda mfupi na mrefu kwa makundi yatokanayo na umri ili kufikia ufanisi unaotarajiwa.  Makundi hayo ni la Watoto wa Umri chini ya miaka mitano, kundi la watu miaka 5 - 17 na kundi la wananchi wa miaka 18 na kuendelea, ambapo Utekelezaji wa Usajili kwa kundi la kwanza umeshaanza kupitia Mpango wa Usajili wa Watoto wa Umri Chini ya Miaka Mitano ambapo kwa sasa unatekelezwa katika Mikoa mitano ya Tanzania Bara ambayo ni Mwanza, Mbeya, Songwe,Iringa na Njombe.
Kaimu Afisa Mtendaji wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Emmy Hudson akizungumza na baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waliofika katika Makao makuu yake Jijini Dar es salalaam leo, wakati akizungumzia Mkakati wa Kitaifa wa Kuboresha Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu hapa nchini.

Kaimu Afisa Mtendaji wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Emmy Hudson akiendelea kuzungumza na wanahabari hao.
Mkurugenzi wa TEHAMA wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Cuthbert Simalenga akifafanua jambo katika Mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad