HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 3, 2017

Raia wa Tanzania na Ufaransa watekwa nyara mashariki mwa DRC

Raia mmoja wa Tanzania, Ufaransa na wengine watatu raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC wametekwa na wapiganaji wenye silaha mashariki mwa nchi hiyo.

Uongozi wa mgodi wa dhahabu wa Banro Corporation ulioko Namoya, umesema kuwa miongoni mwa raia waliotekwa yupo raia mmoja wa Ufaransa, mtanzania mmoja na wengine watatu ni raia wa DRC.

Wapiganaji kutoka kundi la Raia Mutomboki waliwateka raia hao na kukimbia nao msituni huku wakiwatishia kuwaua raia wengine waliojaribu kuwazuia kutekeleza utekaji huo, ameongeza afisa wa eneo hilo Balthazar Hemedi Kabemba.

Wapiganaji hao wametaka kulipwa kiasi kikubwa cha fedha pamoja na mkataba wa ahadi ya kutengenezewa barabara na kuendelea miundo mbinu mingine ya kijamii kwenye eneo hilo.

Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa imesema tayari imeanza mawasiliano na maofisa wa mgodi huo kupata taarifa ya kile kilichotokea.

Mwezi uliopita polisi watatu na moiganaji mmoja walikufa wakati yalipotokea makabiliano na majambazi waliojaribu kuvamia mgodi mwingine wa Twangiza.CHANZO: RFI Kiswahili

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad