HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 30, 2017

MKE WA RAIS MAMA JANETH MAGUFULI AHANI MSIBA WA SIR GEORGE KAHAMA JIJINI DAR ES SALAAM

  Mke wa Rais Mama  Janeth Magufuli akimpa pole Mama janeth Kahama, Mjane wa mwanasiasa  mkongwe na Waziri wa Kwanza wa Ushirika na Masoko katika Baraza la Mawaziri chini ya Serikali ya Madaraka na baadaye Waziri wa Kwanza wa Mambo ya Ndani baada ya  Uhuru, Marehemu Clement George Kahama maarufu kama `Sir George Kahama' aliyefariki dunia hivi karibuni jijini Dar es salaam. 
 Mke wa Rais Mama  Janeth Magufuli akishiriki katika sala na Mama Janeth Kahama, Mjane wa mwanasiasa  mkongwe Marehemu Clement George Kahama maarufu kama `Sir George Kahama’ na ndugu, marafiki na jamaa wa familia ya marehemu aliyefariki dunia hivi karibuni jijini Dar es salaam.
 Mke wa Rais Mama  Janeth Magufuli akiweka saini kitabu cha maombolezo baada ya kumfariji  Mama Janeth Kahama, Mjane wa mwanasiasa  mkongwe na Waziri wa Kwanza wa  Ushirika na Masoko katika Baraza la Mawaziri chini ya Serikali ya  Madaraka na baadaye Waziri wa Kwanza wa Mambo ya Ndani baada ya Uhuru, Marehemu Clement George Kahama maarufu kama  `Sir George Kahama'  aliyefariki dunia hivi karibuni jijini Dar es salaam. Wengine katika picha kutoka kulia ni Mama Janeth Kahama, Mama Evelyn Warioba, Anna Kahama-Rupia, Mama Rahma Bomani,Mama Getrude Luangisa, Mama Ishengoma, Mama Feruzi na Mama Tunu Mwapachu.
Mke wa Rais Mama  Janeth Magufuli akiagana baada ya kumpa pole  Mama Janeth Kahama, Mjane wa mwanasiasa  mkongwe Marehemu Clement George Kahama maarufu kama `Sir George Kahama’ aliyefariki dunia hivi karibuni jijini Dar es salaam.

PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad