HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 25, 2017

MATUKIO KATIKA PICHA: MECHI YA TAIFA STARS DHIDI YA BOTSWANA, SAMATTA ATUPIA MBILI KAMBANI

Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Sammata akiruka juu kushangilia goli lake la kuongoza dhidi ya wapinzani wao Timu ya Taifa ya Botswana, katika mchezo wa kirafiki wa rekodi ya Fifa, uliochezwa jioni hii katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Sammata ameweza kuipachikia timu ya Taifa bao hilo katika dakika ya tatu ya mchezo huo na kuwaacha wa Botswana wakiduwaa na kuanza kumkaba wanne wanne

Mchezo uliendelea kwa timu zote kufanya mashambulizi ya kuviziana kiufundi zaidi huku Stars ikisumbua sana ngome ya Botswana ambayo ililemewa kabisa kwa kosa kosa nyingi kutoka kwa washambuliaji wa Tanzania .

ilipotimu dakika ya 87 mshambuliaji wa kimataifa Mbwana Sammata akapicha bao la pili mara baada ya wa Botswana kucheza faulo na Mshambuliaji huyo kupewa apige faulo.

Mbwana Sammata au kama watu wanavyopenda kumwita Samagoal amewza kuwa nyota wa mchezo wa leo kwa kuisumbua ngome ya Botswana.
 Kikosi cha Taifa Stars kilichoanza leo.
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Botswana.
Mbwana Sammata akiwa ametuliza mpira gambani mbele ya beki wa Botswana ,Ofentse Nato
 Mbwana Sammata akimtoka beki wa Botswana, Ofentse Nato

 Mbwana Sammata akipiga mpira langoni mbeleya mabeki wa Botswana
 Mbwana Sammata akishangilia bao
 Mbwana Sammata akishanngilia


Wachezaji wa Taifa Stars wakishangilia bao
 Shiza kichuya akitawala mpira mbele ya beki wa Botswana Tapiwa Gadibolae

 Ibrahim ajib akiwania mpira wa juu
 Kiungo wa Timu ya Taifa Stars, Himid Mao akiruka juu sambmba na Beki wa Botswana kuwania mpira wa juu, katika Mchezo wa kirafiki wa rekodi za FIFA, uliochezwa jionu ya leo katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam leo. Taifa Stars imeshinda bao 2-0.
 Simon Msuva akitawala mpira
 Shiza kichuya na mpira
 Beki wa kati wa Botswana , Mosha Galemonthale akimchezea vibaya Mbwana Sammata
 Mbwana Samata akiondoka na mpira.














No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad