HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 10 March 2017

Mahakama yaidhinisha kuondolewa madarakani kwa rais Park Geun-hye wa Korea Kusini

Mahakama ya katiba nchini Korea Kusini hatimaye imekubali kuondolewa madarakani kwa rais aliyekuwa amesimamishwa, Park Geun-hye, ambaye anakuwa rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia, kulazimishwa kuondoka madarakani.

Majaji wa mahakama ya katiba kwa kauli moja wameidhinisha uamuzi wa bunge la nchi hiyo kumuondoa madarakani rais Geun-hye, kutokana na ushiriki wake katika masuala ya rushwa yakimuhusisha rafiki yake wa karibu Choi Soon-sil.

Kwa uamuzi huu sasa, inamaana kuwa anapoteza kinga zote za urais alizokuwa nazo na huenda akakabiliwa na mashtaka.
Rais alivuliwa madaraka, Park Geun-hye
Kumeshuhudiwa makabiliano ya polisi na wafuasi wa Park nje ya mahakama ya katiba, ambapo wafuasi wake wanapinga kiongozi wao kuondolewa madarakani na wanapinga uamuzi huu wa mahakama.

Shirika la habari la Korea Kusini Yonhap, limeripoti kuwa watu wawili wamekufa, akiwemo mzee mmoja ambaye alianguka kutoka kwenye gari la polisi, hata hivyo taarifa zaidi bado zinaendelea kuibuka.

Uamuzi huu wa mahakama ni hitimisho la miezi kadhaa ya maandamano yaliyoanza mwaka jana dhidi ya utawala wa rais Park Geun-hye.

Park alisimamishwa kazi za urais toka mwezi Desemba mwaka jana baada ya bunge kupiga kura kutaka aondoke madarakani, huku waziri mkuu akikaimu majukumu yake.

Kwa uamuzi huu wa mahakama una maanisha kuwa nchi ya Korea Kusini itahitajika kuchagua rais mwingine mwanzoni mwa mwezi Mei mwaka huu.

Kwa wakati huu rafiki wa Park, Choi ameshashtakiwa kwa makosa ya kutoa hongo na kwamba alitoa shinikizo kwa makampuni makubwa kutoa fedha ili yapate msamaha wa Serikali, rais Park amekuwa akituhumiwa kujihusisha kwenye kashfa hii.Chanzo: RFI Kiswahili

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad