HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 30 March 2017

MAHAKAMA KUU YATENGUA HUKUMU YA MBUNGE WA KILOMBERO, PETER LIJUALIKALI

Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam imetengua hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya Kilombero dhidi ya Mbunge Peter Lijualikali baada ya kukubaliana na warufani kwamba hati ya mashtaka iliyomtia hatiani ilikuwa na upungufu.

Mbunge Lijualikali alihukumiwa kwenda Jela Miezi Sita(6) bila faini na Mahakama ya Kilombero. Alikuwa akikabiliwa na Kesi ya kufanya vurugu wakati wa Uchaguzi 2015.

Uamuzi huo umetolewa leo mbele ya Jaji Ama- Isaria Munisi baada ya kupitia sababu za kupinga mbunge huyo kutiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela.

Peter aliwakilishwa mahakamani na Wakili Tundu Lissu na Fred Kiwelo wakati Jamhuri ilikuwa ikiwakikishwa na Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi.

Mshtakiwa mwingine aliyehukumiwa kifungo cha nje, Stephani Mgatta adhabu yake pia imetenguliwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad