HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 15 March 2017

KESI YA WEMA SEPETU NA WENZAKE KUSIKILIZWA TENA APRILI 11


Miss Tanzania 2006 na Msanii wa Filamu nchini, Wema Sepetu akiwa katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es salaam leo alipofika kusikiliza kesi inayomkabili ya kukutwa na dawa za kulevya.Upelelezi wa kesi hiyo inayomkabili Wema Sepetu na wenzake wawili haujakamilika, na kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 11 mwaka huu. 

Na Karama Kenyunko.

Upande wa Mashtaka katika kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili msanii marufu wa filamu nchini Wema Sepetu na wenzake wawili umeileza mahakama kuwa upelelezi katika kesi hiyo umefikia hatua za mwisho.

 Mwendesha Mashtaka, Constantine Kakula amedai hivyo leo mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati keai hiyo ilikuwa inatajwa.
"Mheshimiwa hakimu, kesi leo imekuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika ila uko katika hatua za mwisho", amesema Kakula".

Katika kesi hiyo, watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashitaka matatu yanayohusiana na matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi.

 Hati ya mashtaka inadai kuwa Aprili 4, Mwaka huu, katika eneo la Kunduchi Ununio washtakiwa walikitutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya aina ya bangi kiasi cha gramu 1.08.

Miss Tanzania 2006 na Msanii wa Filamu nchini, Wema Sepetu akiwasili  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es salaam leo alipofika kusikiliza kesi inayomkabili ya kukutwa na dawa za kulevya.
Miss Tanzania 2006 na Msanii wa Filamu nchini, Wema Sepetu akitoka mahakamani, baada ya kesi yake ya matumizi ya dawa za kulevya kuahirishwa hadi Aprili 11, mwaka huu. Mwenge suti nyeusi kulia ni mbunge wa Arusha, (Chadema), Godbles Lema akimsindikiza. Nyuma ni wapambe wao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad