HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 7, 2017

Kesi ya wafanyakazi wa Manji sasa Machi 24

Na Karama Kenyunko Blogu ya jamii.
WAFANYAKAZI 16 wa Kampuni ya Quality Group, inayomilikiwa na Yusuph Manji  wanaokabiliwa na tuhuma tano, ikiwemo ya kutaka kutoroka nchini sasa kusomewa maelezo ya awali Machi 24 mwaka huu.

Maelezo hayo yatasomwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya upelelezi wa kesi zao kukamilika.

Wakili wa Idara ya Uhamiaji, Method Kagoma amesema hayo  mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi,  Cyprian Mkeha wakati shauri lilipokuja leo kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa maelezo yao ya awali.

Lakini kabla ya kuwasomea aliiomba Mahakama kubadilisha hati ya mashtaka kwa kuwaongeza washtakiwa wawili ambao walisomewa mashtaka peke yao.

Kuunganishwa kwa washtakiwa hao ambao ni meneja Uwekezaji, Jose Kiran (40) na Prakash Bhatt (35) kumefanya idadi ya washtakiwa hao kufikia 16, pamoja na mashtaka mengine wanadaiwa Pia kuwa, wakiwa raia wa India na waajiriwa wa Kampuni ya Quality Group walimzuia Ofisa wa Idara ya Uhamiaji kutekeleza majukumu yake Februari 20, mwaka huu.

Inadaiwa kuwa katika tarehe hiyo washtakiwa hao wakiwa jijini Dar es Salaam, walimzuia Ofisa huyo ambaye alitaka kutoa taarifa katika makao makuu ya Idara ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam kwamba watu hao wanataka kutoroka kupitia mpaka wa Horohoro,  
Upelelezi wa kesi hiyo umkamilika na imeahirishwa hadi Machi 24,mwaka huu kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Mbali ya wawili hao washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni  Rajat Sarkar (35), Jagadish Mamidu (29), Niladri Maiti (41) Divakar Raja (37) ambao ni washauri wa kampuni hiyo, huku Mohammad Shaikh (44) mhasibu na Pintu Kumar (28) ambaye ni Meneja msaidizi wa kampuni.

Wengine ni Bijenda Kumar (43), Prasson Mallik (46), Nipun Bhatt (32), Anuj Agarwal (46), Varun Boloor, Arun Kateel (46), Avinash Chandratiwari (33) na Vikram Sankhala (50) ambao wote ni washauri wa kampuni hiyo.
Baadhi ya Wafanyakazi hao wa kampuni ya  Quality Group walipopandishwa mahakamani kwa mara ya kwanza,Mahakama ya Kisutu jijini Dar

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad