HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 13 March 2017

KAMATI YA UTALII WATEMBELEA YALIYOKUWA MAFICHO YA MWALIMU NYERERE WAKATI WA HARAKATI ZA UHURU MKOANI MBEYA, IJUE HISTORIA YA MTAA WA "SOKO MATOLA"JIJINI MBEYA.

Kamati ya Utalii ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya ikiongozwa na Afisa Utalii wa Jiji Bi.Levina Modest na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.Geofrey Kajigili wanaofanya kampeni hii kabambe ya utambuzi wa Vivutio vyote vilivyopo Jijini Mbeya kwa kushirikiana na asasi zisizo za kiserikali za Uyole Cultural Tourism Enterprise pamoja na Elimishawamemtembelea Mzee Mkongwe wa Siasa nchini, Mzee Rashid Ally Sinkala ambaye amewahi kuwa Diwani wa iliyokuwa ikiitwa Kata ya Soko Matola (sasa Kata ya Maendeleo) kwa miongo kadhaa pia amewahi kutumika kama Meya ya Halmashauri ya Mbeya Mjini.Mzee Sinkala ameiambia Kamati ya Utalii kuwa Miaka zaidi ya 50 iliyopita wakati wa Siasa za Ukombozi wa Tanganyika Enzi za Chama cha Tanganyika African National Union (TANU)Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa akifikia kwenye nyumba ya mwanasiasa Mkongwe mwanamke aliyejulikana kwa majina ya Zaituni Binti Matola.
Binti Matola alitenga chumba kimoja nyumbani kwake kama Maficho ya Mwalimu Nyerere.
Mzee Sinkala alisema,..."nakumbuka mwaka fulani Serikali ya Kikoloni kupitia Askari wake waliivamia nyumba hiyo nyakati za usiku ili wamuangamize lakini walishindwa kwani Binti Matola alimkimbiza Mwalimu Nyerere kwa kumtorosha kupitia njia ya uani hivyo kufanikiwa kunusuru maisha yake".
Kutokana na Uimara wa Binti Matola kama nguli wa Siasa za Ukumbozi na kama mwanamke shupavu alihudumu  Kama kiongozi mwandamizi wa TANU Mkoa wa Mbeya na hii ndiyo ilifanya Mji huo kukua kwa kasi na kutokana na maendeleo hayo ya kiuchumi ilipelekea wanajamii kwenda mitaa hiyo kupata mahitaji mbalimbali kwa kuiita "Soko Matola".
Mzee Sinkala alimalizia kwa kusema pia nyakati hizo Viongozi wa TANU walijenga Jukwaa la Mikutano maalum ya Chama hasa kipindi Hayati Mwalimu Nyerere ajapo ndipo alikuwa akipatumia kuhutubia.
Jukwaa hilo lipo ulipo Ukumbi wa Mikutano wa Mkapa ,ndani ya Kata ya Maendeleo (Soko Matola)Jijini Mbeya ,maarufu kama "Jukwaa la Mwalimu Nyerere"
Mzee Sinkala akiwa mlangoni mwa Chumba maalum alipokuwa akifikia Mwalimu Nyerere ndani ya nyumba ya muasisi wa TANU na mwanamke mashuhuri Hayati Zaituni Binti Matola aliyepelekea maeneo hayo kuitwa "Soko Matola" Jijini Mbeya
Wajumbe wa Kamati ya Utalii Jijini Mbeya wakimsikiliza kwa makini Meya mstaafu wa Halmashauri ya Mbeya Mjini Mzee Sinkala ndani ya nyumba ya kihistoria ya Binti Matola
Mzee Sinkala akibadilishana mawazo na kijana Thobias Omega, Mjumbe wa Kamati ya Utalii na MwanaHabari kutoka Thobias Omega Blog.


Afisa Habari wa Jiji la Mbeya Bi.Jacqueline Msuya, wa kwanza kushoto akiwa na Mwanamitindo Cleopatra wakati wa Ziara ya Kamati ya Utalii kwa Mzee Sinkala mitaa ya Soko Matola,Jijini Mbeya

NIPANGISHENI HIKI CHUMBA:- Mwenyekiti wa Kamati ya Utalii na Diwani wa Kata ya Sisimba Mhe.Geofrey Kajigili akifurahia mbele ya Kamati ya Utalii akiwa mlangoni mwa Chumba cha maficho cha Mwalimu Nyerere ndani ya nyumba ya Bi.Zaituni Matola Jijini Mbeya
Hili ndilo Jukwaa la Kihistoria lililojengwa toka enzi za Serikali ya Kukoloni na lilikuwa likitumiwa zaidi na Hayati Baba wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere liitwalo "Jukwaa la Nyerere" nje kidogo ya Ukumbi wa Mikutano wa Mkapa, Jijini Mbeya

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad