HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 6 March 2017

HOSPITAL YA TAIFA MUHIMBILI KUSIMAMIA UFUNGAJI MITAMBO YA ‘TELEMEDICINE’ MIKOA MITATU

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) katika kusimamia na kuboresha huduma ya dharura kwa watanzania, inasimamia ufungaji wa mitambo ya kisasa ya ‘Telemedicine’ katika mikoa mitatu ikiunganisha Hospitali saba za Morogoro mjini, Turiani, Kilosa, Lindi mijini, Nyangao na Nachingwea na Mafia ambazo zitawasiliana moja kwa moja na Hospitali ya Taifa Muhimbili katika utoaji huduma wake.

Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Tiba wa Hospital ya Taifa Muhimbili, Dkt Hedwinga Swai ambapo pia alieleza kuhusu huduma za wanaojidunga dawa za kulevya kwamba imeanzishwa kupitia idara ya magonjwa ya afya ya akili katika Hospital ya Taifa Muhimbili, Temeke, Mwananyamala na Mnazi Mmoja Zanzibar.
 Mkurugenzi wa Tiba wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt Hedwinga Swai akizungumza na waandishi wa (hawapo pichani) kuhusu  huduma ya wajidunga  dawa za kulevya imeanzishwa kupitia idara ya magonjwa ya afya ya akili katika Hospital ya Taifa Muhimbili, Temeke, Mwananyamala na Mnazi Mmoja Zanzibar.
 Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Hospital ya Taifa Muhimbili, Dkt Julieth Magandi akizungumza na waandishi wa (hawapo pichani) kuhusu upasuaji wa macho kwa kutumia vifaa vya kisasa (cornea cross linking) upasuaji huo ulikuwa haufanyiki nchini kwa sasa unafanyika katika hospitali hiyo.
 Ofisa Uhusiano wa Hospital ya Taifa Muhimbili, John Stephen akifafanua jambo leo kwenye ukumbi wa habari maelezo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Waandishi wa habari wakimsiliza Mkurugenzi wa Tiba wa Hospital ya Taifa Muhimbili , Dkt Hedwinga Swai Mkurugenzi wa Tiba wa Hospital ya Taifa Muhimbili , Dkt Hedwinga Swai

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad